23.8 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Mwalimu afikishwa mahakamani kwa udanganyifu

FLORENCE SANAWA, MTWARA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  mkoani Mtwara imemfikisha mahakamani mwalimu mkuu wa shule ya msingi Masasi , Mwanaidi Mtaka ,kwa kosa la kumdanganya mwajiri wake na kujipatia zaidi ya sh millioni 1.5 kinyume cha sheria.
Akitoa taarifa hiyo Leo Mei 17,kamanda wa Takukuru Mkoani Mtwara ,Stephen Mafipa, amesema mwalimu huyo anatuhumiwa kwa makosa ya kutumia nyaraka zenye maelezo ya uongo kumdanganya mwajiri wake kinyume cha kifungu cha 22 cha sheria ya TAKUKURU. Na.11/2007.

Amesema pia anakabiliwa na kosa la ufujaji wa mali ya umma kinyume cha kifungu cha 28(1) cha sheria ya  kuzuia na kupambana na rushwa Na.11/2007.

“Inadaiwa kuwa mnamo mwezi Julai, 2015 mtuhumiwa akiwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Masasi mkoani hapo alitumia na kuwasikisha stake adha zenye kuonyesha kuwa alitumia jumla ya shilingi millioni 1,578,000/- kununua vifaa mbalimbali kwaajili ya matumizi ya shule huku akijua kuwa hajanunua vifaa hivyo.

”Udanganyifu huo ulimwezesha kujipatia kiasi hicho cha fedha na kuzitumia kwa matumizi yake binafsi jambo ambalo ni kosa kisheria kufanya hivyo na pia ni matumizi Mabaya ya Mali za umma,” amesema Mafipa .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,719FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles