26.5 C
Dar es Salaam
Friday, January 28, 2022

Mwalimu adaiwa ampachika ujauzito mwanafunzi wake

MOHAMED HAMAD-KITETO

JESHI la Polisi Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, linamshikilia mwalimu, Daniel Saulo wa Shule ya Msingi Matui kwa tuhuma za kumpachika ujauzito mwanafunzi wake wa darasa la saba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, RPC Christopher Foime, amethibitisha tukio hilo kwa kukamatwa mtuhumiwa huyo na yuko Kituo cha Polisi Matui kwa ajili ya upelelezi na uchunguzi zaidi.

“Kwa sasa mtuhumiwa tunamshikilia Kituo kidogo caha Polisi Matui, anaendelea na mahojiano, atafikishwa mahakamani wakati wote taratibu zitakapokamilika ili sheria ifuate mkondo wake,” alisema Kamanda Foime.

Akizungumzia tukio hilo Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Victoria Mushi, alikiri kukamatwa mwalimu huyo akisema tukio hilo ni la tatu kujitokeza shuleni hapo  na kwamba hawezi kusema lolote kwa sasa.

“Nilikuwa Kanisani sikupokea mapema simu yako, kuhusu suala hili la mwalimu yupo Polisi kwa sasa siwezi kuzungumzia lolote, ingawa matukio haya yamekuwa yakijirudia ni tukio la tatu, kwahiyo bado siwezi kusema lolote kwa sasa ndugu yangu,” alisema Mwalimu Mushi alipokuwa anazungumza kwa njia ya simu.

Akizungumza na MTANZANIA baba mzazi wa mtoto huyo, Isaka Maro alielekeza masikitiko yake kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Victoria Mushi kwa kuficha tukio hilo ingawa alilifahamu toka mwanzo wiki wiki mbili zilizopita baada ya shule kuwapima wanafunzi hao.

“Taarifa za kuwa mwanangu ana ujauzito wa miezi miwili nilizifahamu toka kwa watu wiki mbili zilizopita ..nilipoenda shuleni kuuliza mwalimu Mkuu alinificha ndipo nikaamua mwenyewe kumchukua mwanangu na kwenda kumpima kwenye kituo cha Afya Engusero na kubaini haya,”alisema

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magesa, alisema tatizo la watoto wa kike kukatishwa masomo kwa kupachikwa mimba limekithiri, pamoja na kuwepo kwa sheria Serikali inaendelea pia kuelimisha umma kuacha kuwapachika mimba wanafunzi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
177,106FollowersFollow
532,000SubscribersSubscribe

Latest Articles