Mwakyembe awaita Watanzania kuhudhuria Jamafest

0
447

Iman Mketema


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amewaita Watanzania kujitokeza kwa wingi kuhudhuria tamasha Tanzania la Jamafest linalotarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 21 hadi 28, mwaka huu jijini Dar es Salaam

.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Septemba 18, Dk. Mwakyembe amesema lengo la tamasha hilo litakalofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ni kulinda na kuhifadhi na utamaduni wa kiafrika na kuweza kutambulika zaidi duniani.


“Hii ni sherehe kubwa sana nchini kwetu kwani wazungu walivuruga utamaduni wetu enzi za utumwa na kupitia tamasha hili tunatunza utamaduni wetu,” amesema Dk. Mwakyembe.


Amesema katika tamasha hilo kutakuwa na wimbo maalumu uliotungwa na msanii Peter Msechu akiwashirikisha wasanii wenzake Mimi Mars, Barnaba, Linah Sanga, Rich Mavoko na Khadija Kopa.


“Lakini pia natoa nafasi ya kutumbuiza kwa msanii Nasibu Abdul (Diamond Platnumz) aje ajiunge na wasanii wenzake waweze kutumbuiza pamoja kwenye tamasha hilo kwani tamasha kama hilo lililofanyika Kenya niliona kulikwa na ushirikiano mkubwa baina ya wasanii hao nchini humo,” amesema Dk. Mwakyembe.


Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dk. Kiagho Kilonzo, alitangaza kuwa kutakuwa na tuzo za filamu kutoka bodi hiyo kwenye tamasha hilo.


“Kutakuwa na tuzo tofauti tofauti kwenye tuzo hizo na ninawaomba wasanii wenye kazi zao wazilete ili zishindanishwe na washindi watatu watapatikana,” amesema Kilonzo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here