Na Mwandishi Wetu       |       Â
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema ni kweli kuna upungufu mkubwa katika uwanja wa taifa ndiyo maana wakaiomba Bunge fedha kwa ajili ya ukarabati.
Kutokana na hilo, amesema tayari Bunge limeidhinisha Sh bilioni moja kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kiwanja cha taifa.
Mwakyembe ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu ambaye amesema katika uwanja wa taifa eneo la VIP hakuna kibanda wakati hali ya hewa inapobadilika.
“Eneo la VIP katika uwanja wa taifa hakuna kibanda ya kuwakinga na jua viongozi na watu wanaokwenda kutazama mpira, je serikali ina mpango gani kujenga mabanda katika eneo hilo,”amehoji.
Akijibu swali hilo, Mwakyembe amesema:”Ni kweli kuna upungufu katika uwanja wa taifa ndiyo maana tukaomba fedha kwa ajili ya ukarabati ili ukidhi na kuendana na viwanja vya FIFA.
“Bunge hili tukufu limeidhinisha Sh bilioni moja ili itumike kuboresha miundombinu ya kiwanja cha taifa,”amesema.