23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 10, 2022

Mwakinyo: Nitamkalisha Tinampay

Na GLORY MLAY

BONDIA Hassan Mwakinyo, amesema kwa maandalizi anayofanya atajhakikisha anamkalisha chini bondia Arnel Janiola Tinampay raia wa Filipino raundi ya kwanza, katika pambano litakalifanyika Novemba 29, mwaka huu.

Pambano hilo la uzito wa kilo 69 la raundi 10 limepangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ambalo litatanguliwa na mapambano matano.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwakinyo ambaye ameweka kambi yake mkoani Tanga, alisema maandalizi yake yanaendelea vizuri hivi sasa kwani anazingatia ushauri aliopewa na mwalimu wake ambapo amemtaka afanye mazoezi pamoja na kuchukua mapumziko.

Alisema naamini atampiga Tinampay kwani anaamini hakuna bondia anayeweza kumfikia kwa sasa kwa uwezo na kiwango alichonacho na lengo lake katika pambano hilo ni kuendelea kuweka rekodi za kuwapiga mabondia wa kubwa.

“Nataka kuendelea kufanya vizuri ndio sababu nimeamua kuja kuweka kambi huku ili kufanya maandalizi ya nguvu, naomba tu mashabiki na wadau wa ngumu wajitokeze kwa wingi siku hiyo kushukudia nikitoa kichapo kwa mpinzani wangu huyo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,395FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles