23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mwaka mpya wa Kiislamu uwe wa mabadiliko – Sheikh Jalala

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Waumini wa dini ya Kiislamu wametakiwa kuendelea kuenzi umoja na mshikamano wa kitaifa katika mwaka mpya wa Kiislamu 1445.

Mwaka Mpya wa Kiislamu ni siku muhimu katika kalenda ya Kiislamu duniani kote na huadhimishwa kila mwaka.

Wito huo umetolewa Dar es Salaam Julai 18,2023 na Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithnashaari, Hemed Jalala, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwaka mpya wa Kiislamu.

Amewataka waislamu wajitathmini mwaka uliopita wapi wamefanikiwa, walikokwama na namna watakavyoweza kusonga mbele.

Sheikh Jalala pia amesisitiza mwaka mpya wa kiislamu uwe wa kuenzi umoja wa Watanzania wote bila kujali tofauti zao na dini zao.

“Mwaka 1445 uwe ni mwaka wa umoja, mshikamano, tuungane na kuwa kitu kimoja na kuhimiza umoja. Waislamu umefika muda wa kuacha tofauti zetu na kukaa meza moja.

“Umoja wa Watanzania ni muhimu mno, umoja wa kitaifa, kupenda Tanzania yetu ni moja kati ya misingi muhimu. Tuhubiri umoja kati ya sisi waislamu na ndugu zetu wakristo, tuhakikishe dini hizi zinashikamana, zinakaa vizuri na zinapendana,” amesema Sheikh Jalala.

Amewahimiza viongozi wa dini kuhubiri zaidi kuhusu mmomonyoko wa maadili ili vijana wawe na maadili mema yanayompendeza Mungu.

Waislamu wanasherehekea mwaka mpya wakimkumbuka pia Imamu Hussein ambaye aliuawa akipigania kurudisha maadili, mshikamano, umoja na amani katika jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles