MDOGO wake na Kim Kardashian, Khloe, amesema mwaka huu wa 2015 unaoelekea ukingoni, umekuwa mbaya kwake kutokana na kukumbwa na majanga mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpenzi wake kuugua.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, mrembo huyo aliandika kuwa, amepatwa na mitihani mingi lakini kubwa zaidi ni kuugua kwa mpenzi wake Lamar Odom kwa kipindi kirefu.
“Hauwezi kuwa na raha na amani kama mtu wako wa karibu yupo hospitali, nimekuwa na wakati mgumu kwa kuwa mpenzi wangu Lamar bado yupo hospitali, japokuwa anaendelea vizuri lakini naweza kusema huu ni mwaka mgumu kwa upande wangu,” aliandika Khloe.