27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mvuvuma kuivaa Abajalo Daraja la Pili leo

NA MWANDISHI WETU

KIVUMBI cha Ligi Daraja la Pili kinaendelea leo katika viwanja tofauti huku timu ya Mvuvuma FC ikiikaribisha Abajalo FC ya Tabora katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Jumla ya timu 24 zitakuwa katika viwanja 12 tofauti kusaka nafasi nne za kupanda Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Baraka Kizuguto, alisema kuwa katika mchezo mwingine Transit Camp watacheza dhidi ya Mirambo FC katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga huku Singida United watawakaribisha Green Warriors katika Uwanja wa Namfua mjini Singida.

Kundi B, Alliance FC watawakaribisha AFC ya Arusha katika Uwanja wa CCM Kirumba, JKT Rwamkoma watacheza dhidi ya Madini FC katika Uwanja wa Karume Musoma, Kundi C Changanyikeni dhidi ya Kariakoo ya Lindi watacheza katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Mechi hizo zitaendelea kwa Kundi D ambapo African Wanders watawakaribisha Sabasaba FC katika Uwanja wa Wambi, Mafinga wakati Mkamba Rangers watacheza dhidi ya Mbeya Warriors katika Uwanja wa CCM Mkamba na Wenda FC watacheza dhidi ya Mighty Elephant katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo mitatu kuchezwa katika kundi B na C, Pamba FC watawakaribisha Bulyanhulu FC katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mshikamo watacheza dhidi ya Abajalo katika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi na Villa Squad watachuana na Comsopolitan katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles