24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mvua zasababisha wagonjwa kukosa matibabu

NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM

MVUA zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimesababisha kukatika kwa mawasiliano ya Mtaa wa Kisiwani Kata ya Bonyokwa Manispaa ya Ilala na kusababisha wagonjwa kushindwa kwenda kupata huduma katika Zahanati ya Bonyokwa.

Mtaa huo, una wakazi 600,000 na kwa siku zahanati hiyo inahudumia wagonjwa kati ya 30 hadi 50, huku kwa mwezi ikihudumia wagonjwa 700.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Dar es Salaam jana, baadhi ya wakazi wa mtaa huo walisema kero hiyo imedumu kwa muda mrefu na hadi sasa hakuna utatuzi wowote uliofanywa.

“Magari, pikipiki haziwezi kupita na ikitokea tukapata dharura ya mgonjwa kama mjamzito ni changamoto kwa sababu hata gari la wagonjwa halitaweza kufika zahanati,” alisema mmoja wa wakazi hao,Fortunatus Masimami.

Mkazi mwingine, Willy Kamwela alisema kutokana na kuharibika kwa barabara hiyo wanalazimika kuacha magari yao umbali mrefu na nyumba zao na kuingia gharama ya kulipa Sh 2,000 kila siku ya ulinzi.

“Wanafunzi wanashindwa kufika shule kwa wakati kwa sababu hata bodaboda au magari hayawezi kufika huku,” alisema Kamwela.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kisiwani, Peter Mwasingi, alisema awali alifuatilia kwa Wakala wa Barabara (TANROADS) lakini aliambiwa kuwa barabara hiyo ipo chini ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ambao walisema kwa sasa haijatengewa fedha.

“Kero hii imekuwa ikitokea mara kwa mara na nimekuwa nikichukua hatua mbalimbali, nilikwenda Tanroads kufuatilia walikuja hapa kukagua lakini wakasema barabara hii ipo chini ya Tarura.

“Nilipowafuata Tarura walisema hawana fedha, imekuwa ni danadana tu lakini mwisho wa siku wananchi ndio wanaopata shida,” alisema Mwasingi.

Alisema kijografia zahanati hiyo iko mlimani hivyo kufikika inategea barabara hiyo.

Alisema walijadiliana na wananchi na kukubaliana kuchangishana Sh 50,000 kwa kaya zinazoishi pembezoni mwa barabara hiyo ili kumwaga kifusi kuwezesha ipitike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles