23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Mvua zaacha balaa Dar, mikoani

Na Nyemo Malecela, Kagera

MVUA zinazoendelea kunyesha Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, zimeleta uharibufu wa mali na miundombinu, ambayo jana barababara kadhaa za jijini Dar es Salaam zilifungwa kwa muda kutokana kujaa maji.

Aprili 15 TMA ilitoa taarifa iliyoonyesha Aprili 16 na 17 kutakuwa na mvua kubwa Dar es Salaam ambayo ilitarajiwa kuongezeka zaidi Aprili 18 na 19.

Kutokana na mvua hiyo, haswa iliyonyesha kuanzia juzi usiku hadi jana, baadhi ya nyumba zilianguka huku maeneo mengine kuta za fensi zikianguka.

Jana MTANZANIA ilizunguka maeneo mbalimbali Dar es Salaam ikiwamo Tabata Kisiwani, Kigogo, Jangwani, Mkwajuni na kushuhudia baadhi ya nyumba zikiwa zimengukwa na maji.

Pia wanaotumia usafiri wa mwendo kasi, waliathirika zaidi kutokana na kufungwa kwa barabara ya Jangwani na Mkwajuni, ambapo safari zilizokuwa zikifanyika zilikuwa kati ya Morocco na Kimara na Fire kwenda katikati ya Jiji.

Akizungumza na Mtanzania, mkazi ya Buza wilayani Temeke, alisema mvua hizo ziliangusha nyumba ya jirani yake ikiwa ni muda mfupi baada ya majirani kuwatoa watoto waliokuwamo ndani.

“Tulikuwa tumelala kwenye saa saba usiku tukasikia watoto wanapiga kelele wakisema wanakufa, tulitoka baadhi ya majirani tukawaambia watoke nje kisha wakaingia kwenye nyumba ya jirani yetu mwingine, niliporudi kulala hata nusu saa haijapita nikasikia kishindo, kumbe ni nyumba waliyokuwa wale watoto ndo ilianguka.

“Na mimi leo (jana) nimetoka nyumba vizuri pakiwa salama, nafika njiani msichana wangu wa kazi ananipigia siu ananiambia ukuta wa nyumba yangu umeanguka,” alisema Nora Desi.

Pia eneo la Jangwani, watu ambao nyumba zao zimezingira na maji, walionekana kukaa pembezoni mwa barabara wakiwa wametengeneza mahema ya mifuko.

Kagera

Mkoani Kagera imeelezwa kuwa magugu maji yaliyoziba daraja la Bukoba Club, yamesababisha mafuriko katika mitaa inayozunguka mto Kanoni unaokatiza mitaa ya Manispaa ya Bukoba.

Godfrey Sosipiter alisema ameishi katika mtaa wa Bukoba Inn tangu mwaka 1993 lakini kabla ya daraja hilo kuzibwa na magugu maji walikuwa hawapati mafuriko.

“Sababu kubwa ya mafuriko haya ni daraja la Bukoba Club ambapo limezibwa na magugu maji. Tayari tulishamueleza mkurugenzi tatizo la daraja hilo akatuahidi atatuletea vifaa vya kusafisia na alivyozibua maji yakaisha, sasa leo mvua ilivyonyesha maji yakajaa na hii ni kutokana na daraja hilo kuzibwa na magugu maji.

“Tunaomba kitengo kinachoshughulikia mazingira watusaidia kutuondolea hii adha ya maji kuacha njia yake ya asili na kuingia kwenye makazi ya watu,” alisema.

Naye Paschal Thimos mkazi wa Mtaa wa Sure Road alisema tangu miaka ya 1993 mto huo ulikuwa na kina kirefu sana lakini hivi sasa umejaa mchanga na magugu maji na kusababisha maji kushindwa kupita inavyotakiwa.

“Tunaomba walisafishe daraja hilo ili maji yaweze kurudi kwenye njia yake ya kuelekea katika Ziwa Victoria,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawilo, alipoulizwa ni hatua gani zinachukuliwa ili kusafishia daraja hilo alisema “wewe huoni mvua zinanyesha alfu we unasema daraja, daraja maana yake nini?

“ Wewe ni mwandishi wa habari fanya utafiti wako, kila mahali Dar es Salaam maji, nchi nzima maji, kadaraja haka ndio kanaweza kusababisha adha yote hii?

“Yaani hamuoni kwamba Ziwa Victoria maji yameongezeka yamejaza kila mahali alfu mnasema daraja, what is this? We nenda huko kaangalie daraja auangalie ziwa lilivyo, wewe si mwandishi wa habari uliyesoma?” Alisema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,426FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles