27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, November 7, 2024

Contact us: [email protected]

MVUA YASABABISHA KAYA 56 KUKOSA MAKAZI

Na Omary Mlekwa, Hai

Kaya 14 zimekosa makazi katika Kijiji cha Kawaya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na nyingine 42 nyumba zao zikiharibiwa vibaya na mvua iliyonyesha juzi ikiambatana na upepo mkali.

Mvua hiyo iliyonyesha kwa takribani saa tatu, mbali na madhara hayo pia ilisababisha uharibifu wa miundombinu mbalimbali pamoja na kuzoa chakula kilichokuwa kimehifadhiwa ndani katika maghala ya vitongoji vya Kilimamswaki na Mbuguni.

Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo, Kipi Warioba ametembelea eneo hilo ambapo amesema hadi sasa kaya 14 zimehifadhiwa na wasamaria wema kutokana na kukosa makazi.

“Mvua hiyo imesababisha madhara makubwa, wananchi waliopata maafa wamehifadhiwa kwa majirani baada ya uongozi wa kijiji kufanya utaratibu wa kuhakikisha kuwa wananchi hao wanapata huduma zote zinazostahili nawapongeza kwa juhudi hizo, ”amesema Warioba.

Hata hivyo pamoja na mambo mengine, Warioba amesema uchunguzi wa awali katika kijiji hicho, umeonesha kuwa sehemu ambazo zimepata maafa hayo hazina miti ya kutosha kuzuia kasi ya upepo kuelekea kwenye makazi ya wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles