29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MVUA YAPANDISHA BEI YA VYAKULA KARIAKOO

Na FERDNANDA MBAMILA-DAR ES SALAAM

ONGEZEKO la bei ya bidhaa kipindi hiki cha sikukuu katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam, kimesababishwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili jana kwa nyakati tofauti, Ofisa Masoko wa soko hilo, Henry Gwajina, alisema bei ya mazao imekuwa ikipanda siku hadi siku kutokana na mvua nyingi kunyesha mfululizo.

Alisema bei zimeongezeka hasa katika upande wa vyakula kama vile vitunguu, viazi, mchele, unga na bidhaa nyingine ambapo kwa gunia la viazi la kilo 75 hadi 80, linauzwa kwa kiasi cha Sh 100,000 wakati bamia mfuko mmoja ni Sh 85,000.

“Biashara ya kuuza bidhaa sokoni imekuwa ngumu sana ukilinganisha na ilivyokuwa hapo awali, hiyo ni kutokana na bidhaa nyingi kutokutoka kimauzo kwa kipindi hiki,” alisema Gwajina.

Alisema kwa upande wa wafanyabiashara wanajitahidi wawezavyo ili kwa siku warudi na chochote kuliko kukaa bila kufanya biashara kabisa.

Gwajina aliwaomba wakulima kuchukulia hii hali kuwa ni janga la wote na kuweza kuwapunguzia gharama wafanyabiashara pale wanapokwenda kununua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles