27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mvua ya vuli yaanza kwa kishindo

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi.

JOHANES RESPICHIUS, Dar es Salaam

MVUA ya vuli iliyoanza kunyesha juzi katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam,  ilianza kwa kishindo na kusababisha adha kubwa ya usafiri katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

Mvua iliyoanza kunyesha usiku wa kuamkia juzi, ilisababisha baadhi ya barabara za Morogoro, Sam Nujoma na Ally Hassan Mwinyi kuwa na foleni iliyosababisha watu kuchelewa kazini.

Akizungumza na MTANZANIA kuhusu mvua hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi, alisema ilitarajiwa kunyesha kwa vile  hiki ni kupindi cha vuli.

“Kipindi cha kuanzia Oktoba hadi Desemba huwa ni kipindi cha mvua za vuli, kwa hiyo mvua hii ilitarajiwa kunyesha, hata utabiri wa TMA jana (juzi) ulibainisha suala hili,” alisema Dk. Agnes.

Alirejea taarifa za msimu wa mvua ya vuli ya Oktoba hadi Desemba, akisema katika msimu huu kunatarajiwa kupata mvua chache katika maeneo mengi ya nchi huku sehemu nyingine ikichelewa kunyesha.

Alisema kutokana na uchache wa mvua inayotarajiwa kunyesha, kunaweza kusababisha athari za ustawi wa mazao ya kilimo kwa vile  unyevunyevu katika udongo unaweza kupungua.

“TMA inashauri sekta ya afya kuchukua hatua stahiki kupunguza athari  inayoweza kujitokeza kwa sababu  milipuko ya magonjwa inaweza kutokea kutokana na uhaba wa maji salama na matumizi mabaya ya mifumo ya maji mijini.

“Licha ya kuwa na vipindi vichache vya mvua, kuna uwezekano wa matukio ya vipindi vya mvua kubwa kusababisha  mafuriko katika maeneo yasiyo na uoto wa asili,” alisema Dk. Agnes.

Mkurugenzi huyo aliwashauri wakulima kuandaa mapema mashamba na pembejeo pamoja na kuzingatia ushauri wa maofisa ugani wa kilimo kwa matumizi sahihi ya ardhi na mbegu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles