30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Muungano hautavunjwa-Shaka

Mwandishi Wetu, Morogoro

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro, kimesema hakuna mtu, watu au kikundi chochote cha nje au ndani ambacho kina misuli, ubavu na jeuri ya kuutikisa na kuusambaratisha Muungano waTanganyika na Zanzibar uliiofikisha miaka 56 mwaka huu. 

Imesema mtu mwenye ndoto, fikra au nia ya kutaka kuwagawa Watanzania walioungana kwa ridhaa na sasa wakiwa na umbile moja, atashindwa kwasababu nguvu za muungano kidola na kijeshi ni kubwa kuliko ilivyokuwa Aprili 26, 1964 .

Matamshi hayo yalitolewa juzi na Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na wandishi wa habari kutoa mtazamo wake juu ya uwepo wa Muungano. 

Alisema wapinzani wa Muungano, hawakuaanza visa, chochochoko na vituko juzi , jana na leo , mchakato wa kuundwa muungano uliianza kupingwa na vibaraka wachache hata kabla ya kuundwa kwake ila njama hizo hazikufua dafu na kuvia kutokana na nguvu thabit za uzalendo. 

Alisema hata wakati ambao vyama ukombozi vilipokuwa vikishiriki  vikao vya umajumui (Pan Africanism ), zipo taarifa  walikuwepo baadhi ya viongozi na vyama vyao walioitikia kwa shingo upande na kusaini azimio la kuundwa dola moja ya Afrika, baada ya nchi zao kupata uhuru huku mioyo yao ikiwaza madaraka na vyeo badala ya kufikiria umoja wa Afrika na maendeleo ya watu wake kiusalama na kichumi. 

“Mtu sasa anapofikiria muungano kwamba siku moja utavunjika, utasambaratika na Watanzania watagawanyika , ndoto hizo ni batili na zinaweza kumtokea mtu juha au mwehu akiwa usingizini , mwenye fikra njema na yakinifu hawezi kutokewa na njozi za aina hiyo,”alisema. 

Alisema i baada ya miaka 56 kupita sasa, mwananchi wa Makunduchi Mkoa Kusini Unguja, anaishi Kamachumu mkoani Kagera, aliyezaliwa Ileje Mbeya ameoa mke anayetoka vitongoji Pemba au mtu wa Loliondo ameweka makazi ya kudumu kule Bwejuu au Donge kamwe muungano huu hautavunjika hata kwa bahati mbaya.

“Tumeziunganisha nchi zetu mbili huru kwa ridhaa, makubaliano na nia njema, toka ulikuwa mwaka mmoja wa madhimisho ya Muungano sasa imefika miaka 56, hatutakubali kurudishwa nyuma kwa mayowe ya wasaka madaraka na mawakala wafalsafa ya ubeberu mamboleo “Alieleza Shaka 

Alisema hata unapoutazama upande wa pili wa muungano,marais wamekuwa wakibadilishana madaraka ya utawala bila kuwepo longolongo au mivutano tokea awamu ya kwanza hadi sasa awamu ya saba chini ya Rais wa Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein. 

Alisema siku zote eneo hilo litaendelea kutii, kufuata, kuheshimu na kuisimamia ipasavyo misingi ambayo imeuunda muungano wa Tanganyika na Zanzibar bila kutetereka. 

“Muungano wetu umewashangaza walimwengu duniani kwa kitendo cha kudumu kwake, kuwaunganisha wananchi wake na kuwa wamoja, wenye upendo na mshikamano pia wasiofuata udini, ubaguzi wa rangi na ukabila, hiyo ndiyo fahari ya muungano na Tanzania yetu “Alisisistiza Shaka. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles