29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Muuguzi adaiwa kubaka mjamzito chumba cha kujifungulia

Walter  Mguluchuma Katavi .

MKAZI wa Kijiji cha Majimoto wilayani Mlele mkoani Katavi, jina lake limehifadhiwa mwenye umri wa miaka 22, anadaiwa kubakwa na muuguzi wa   wa kituo cha afya Mamba, Abednego Alfred (32), wakiwa ndani ya chumba cha  kujifungulia.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi,Benjamin Kuzaga  alisema tukio hilo la kinyama na la kikatili  lilitokea Desemba  18, mwaka huu saa 2 usiku katika chumba cha kujifungulia wajawazito.

 Alisema siku ya tukio, mwanamke huyo  alipatwa na uchungu wa kujifungua baada ya siku zake kutimia, alitoka nyumbani kwake Majimoto  kwenda kupata huduma kituoni hapo, huku akisindikizwa na mama yake mzazi .

Baada ya kufika kituoni alipokelewa na    Alfred ambaye aliyekuwa muuguzi wa zamu siku hiyo.

Alisema muuguzi alianza kumpatia huduma ya uzazi, lakini mwathirika wa tukio hilo alihisi  hali isiyo ya kawaida  sehemu zake za siri  hali ambayo ilimfanya ashituke .

Alisema  baada ya kubaini hilo na kuingiliwa licha ya kuwa hatua za mwisho kujifungua alipiga kelele.

Alisema baada  kuona hivyo,  mjamzito aliamua  kuinuka  kitandani  na kwenda  moja kwa moja  kutoa taarifa  kwa  mama yake mzazi, Mektilida  Deogratius  ambaye alitoa taarifa kwa uongozi wa kituo.

Mtuhumiwa baada ya kufanya kitendo hicho, alitokomea kusikojulikana, lakini polisi kwa kushirikiana na walifanikiwa kumkamata.

 Kamanda Kuzaga, alisema  mtuhumiwa   anaendelea kushikiriwa na anatarajiwa  kufikishwa mahakamani  wakati wowote  ili akajibu  tuhuma hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles