24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Muswada wa Sheria ya vileo wapingwa Zanzibar

Mwandishi Wetu -Zanzibar

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi, wameupinga Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Vileo uliowasilishwa mwishoni mwa wiki katika kikao cha Baraza la Wawakilishi na Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ, Haji Omar Kheir.

Wakati wakichangia muswada huo wajumbe wengi waliukataa kwa madai kwamba haujitoshelezi katika kudhibiti athari mbaya za ulevi na ongezeko la baa katika Visiwa vya Zanzibar.

Akichangia kwa hisia kali musada huo, Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae, Mohammed Said Mohammed “Dimwa”, alisema kuwa Serikali imeleta muswada huo baada miaka karibu 92 lakini bado hauoneshi udhibiti makini wa vitendo vya ulevi na ongezeko la baa nchini.

“Mwenyezi Mungu akusamehe Mheshimiwa Waziri na Kamati ya Sheria iliyopitia muswada huu, umemebeshwa msalaba huu peke yako, sheria zote zinaletwa humu Mwenyekiti wa bodi anateuliwa na rais, lakini sheria hii tu bodi yake mwenyekiti anateuliwa na waziri, mimi sitaki kuingia kwenye kumbukumbu ya kupitisha muswada huu, siungi mkono,” alisema Mohammed Said 

Alisema anashangaa muswada huo umeweka adhabu ndogo ya faini ya Sh 500,000 au kifungo cha miezi mitatu kwa watakaofanya biashara za ulevi katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kudai kuwa adhabu hiyo haiwezi kudhibiti kwa vile wafanyabiashara wa pombe wanamudu kulipa hiyo faini.

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Amani, Rashid Ali Juma alisema haungi mkono sheria hiyo kwa vile alitegemea ingekuja kuweka udhibiti na marufuku ya Biashara hiyo kwa vile jimboni kwake tu baa zimekuwa nyingi sana na maeneo mengine ya nchi.

Mwakilishi wa Jimbo la Konde, Mussa Ali Mussa, alitoa tahadhari kuwa muswada huo siyo wa kuletwa kwa wakati huu kwa namna ulivyo kwa vile haujaweka udhibiti wa kutosha wa biashara holela ya pombe.

Katika mjadala mkali wa muswada  Mwalikilishi Jaku Hashim Ayoub, alishauri Serikali kurudi tena kufanyia marekebisho muswada huo na kuweka masharti yatakayodhibiti ueneaji wa biashara ya pombe mitaani.

“Mheshimiwa waziri nakushauri sana, vipo vifungu humu havijawekewa adhabu, vipo vyengine adhabu iliyowekwa ni ndogo kulingana na ukubwa wa makosa lakini pia muundo wa bodi haujaweka zuwio kwa mtu kutokuteuliwa kuwa mjumbe kama anajihusisha yeye au jamaa yake katika biashara ya pombe,” alisema 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles