22.9 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Muswada wa sheria uuzaji vipimo vya VVU kuwasilishwa bungeni

Aveline kitomary

Serikali inatarajia kuwasilisha muswada wa sheria ya uuzaji wa vipimo vya Virusi vya Ukimwi (VVU) bungeni ambao utaruhusu mtu kupima afya yake mwenyewe  ili kuongeza idadi ya watu watakaopima kutokana na baadhi ya watu kuwa waoga.

Akizungumza katika mafunzo yaliyotolewa kwa wasanii kuhusu Virusi vya Ukimwi na Ukimwi Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kutokana na watu kuogopa  unayanyapaa umefanya watu wengine kushindwa kupima VVU kwahiyo hatua hiyo itasaidia watu kupima na kujua afya zao.

“Watu wengi hawapendi kupima kwasababu pia kuna unyanyapaa tutarekebisha sheria ili watu waweze kujipima wenyewe virusi vya ukimwi lakini mtu atakapojipima tutamshauri aende kituo cha afya kupata vipimo zaidi.

“Nanawashukuru na kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya katika kushiriki ujenzi wa Tanzania ya viwanda kupita sanaa kwani sanaa ni ajira,burudani na biashara.

“Mmekuwa mstari wa mbele kushiriki katika kampeni za kutoa elimu kwa jamii kuhusu ugonjwa wa Ukimwi na jamii kwa kiasi kikubwa wameshaelewa, tumeona iko haja ya kukutana na nyie ili kufanya ushawishi hasa kwa vijana wa kike na kiume hivyo tumekutana kutoa taarifa sahihi kuhusu Ugonjwa huu,”amebainisha.

Ummy amesema malengo makubwa ya Wizara hiyo ni kutokomeza maambukizi mapya ya VVU ifikapo mwaka 2030.

“Na tutafikia malengo hayo kwa malengo ya kimataifa kuwa mwakani 90 ya kwanza tuko asilimi 80 wanafahamu kuwa katika kila watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi wawe na ufahamu kuhusu hali zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,476FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles