23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

MUSWADA WA SHERIA MPYA YA MADAKTARI WAZUA HOFU

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

Na FREDERIC KATULANDA-MWANZA

 MADAKTARI wasaidizi na matabibu wameishauri Serikali kutafakari uamuzi wake wa kutowatambua kama madaktari katika Muswada wa Sheria ya Madaktari, Madaktari wa Meno na Watalaamu wa Afya wa Mwaka 2016, kwa kuwa utasababisha vifo na kuathiri watu wengi kwa kukosa huduma ya afya.

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti, baadhi ya madaktari hao walisema hadi sasa idadi ya madaktari wasaidizi nchini (AMO) ni 3,040 wakati wale madaktari wenye shahada (MD) wakiwa hawafikii hata nusu yao, hivyo wao wamekuwa wakihudumia sehemu kubwa ya wagonjwa.

Akielezea uamuzi wa Serikali juzi, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema kuwa licha ya kuthamini mchango wao wa kutoa huduma za afya nchini, wizara yake imekataa mapendekezo yao ya kuitwa madaktari kwa kuwa sifa muhimu ya kuitwa daktari ni shahada ya kwanza ya udaktari inayotambulika.

Akizungumzia muswada huo, Dk. Donald Musumu, alisema uamuzi wa Ummy katika muswada huo umeonyesha kukataliwa kwa mapendekezo 18 kati ya 37 yaliyowasilishwa na wadau, wakitaka madaktari wasaidizi kuendelea kutambuliwa, hivyo watakoma kuwa madaktari na kutoa huduma.

“Waziri ametamka kuwa katika mapendekezo aliyowasilisha lile la kuwatambua madaktari wasaidizi limekataliwa, hivyo tafsiri yake ni kuwa iwapo muswada huo utapitishwa, basi utawaathiri madaktari wasaidizi wengi ambao watakoma kutoa huduma na kufunga hospitali zilizofunguliwa kwa vyeti vyao.

“Kwa mujibu wa muswada huo, madaktari wasaidizi watakoma kuendelea kutoa huduma na watakaobainika wakitoa huduma na kufanya upasuaji watashtakiwa na kutozwa faini ya shilingi milioni tano, jambo hili Serikali inapaswa kuangalia kwa makini kwa kuwa wamekuwa wakitegemewa kwa huduma za upasuaji wa dharura kwa wajawazito vijijini ambako hakuna madaktari wenye shahada,” alisema Dk. Musimu.

Alisema ni mapema mmno kupitisha sheria inayowaengua AMO kuendelea kutoa huduma na kubaki na MD pekee ambao bado hawatoshelezi mahitaji ya utoaji huduma na kubainisha jambo hilo litaathiri huduma ya afya kwa ujumla.

“Muswada huo unatuita wahudumu shirikishi na kunyang’anywa leseni zetu, hivyo hatutaweza kutibu, ni kwanini Serikali isifikirie upya jambo hili? Kama tulionao hawatoshi kutoa huduma kwa nchi nzima unawapotezaje na hawa kidogo ulionao ambao wamekuwa wakisaidia kuokoa maisha ya Watanzania?” alisema na kuhoji.

 WAJIANDAA KUKUTANA

Akizungumza jana kwa simu, Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Wasaidizi, Madaktari Wasaidizi wa Meno, Matabibu na Matabibu Wasaidizi, (AMEPTA), Dk. Francis Ngonyani, alisema taarifa iliyotolewa na Ummy imewastua madaktari hao na kwamba wanajiandaa kukutana ili kutoa tamko lao.

- Advertisement -

Related Articles

4 COMMENTS

  1. Hii si nzuri italeta mgawanyiko mkubwa ambao utaleta athari kwenye Huduma za Afya,,,,cha msingi Waziri azingatie juu ya ombi la madaktari wasaidizi watambulike kama madktari kamili

  2. Kinachofanywa na serikali ni ukiukwaji wa haki za Amos maana vyuo waliosoma ni vya serikali, na ujuzi waliopata ndo wanategemea kusustain maisha yao sasa gafla unasema huwatambui kw sababu Una Mds wa kutosha? Kitendo hicho mi nafananisha mtu anayemfukuza mke wake wa kwanza aliyesota Naye kw kumpata mke ndogo!

  3. kwa nchi hii kubwa ya tanzania ambayo bado ina kuwa na watu tunaaendelea kuzaliana ni haki kuwa na wataalamu wenye ujuzi mkubwa ili kuweza kusaidia nchi, lakini tunapo fikiri kuwatoa watu ambao tumewaamini kuokoa maisha yetu kwa madai ya taaluma yako mengi yakuyafikiri ikiwa ni pamoja na kufukiri kuboresha huduma za kutendea kazi, taaluma inayo tolewa na zaidi je hao ambao tunawapa taaluma ya shahada wanatosha na wanafanya kama iwapasavyo…… TANZANIA IS BIG COUNTRY AND SHOULD BE SAVE EVEN BY THOSE WITH MINOR KNOWLEDGE THO, We HAVE TO MAKE CHANGE. BUT CONSIDER WHAT YOU HAVE IN HANDS AND TIME. God bless Tanzania

  4. haya yote yanaletelezwa na huyo kijana alueteuliwa kuwa naibu waziri wa wizara hiyo. alianza kwa kumsumbua dr. mwaka sana kisa ni hilo swala kuitwa dr. kwani akiitwa dr na akatoa huduma safi kuna tatizo gani….. mimi namwomba aache ULIMBUKENI WA ELIMU kwa kuwa yeye ni MD asiwe mbinafsi wenzake kuitwa madaktari pia. na aache kumshauri waziri ummy ubaya maana ataonekana hana sifa ya kuongoza wizara hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles