31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Muswada wa ajira waligawa Bunge

Na Fredy Azzah, Dodoma
MUSWADA wa Sheria ya Kazi na Ajira uliosomwa bungeni kwa mara ya pili jana na Waziri wa Kazi na AJIRA, Gaudentia Kabaka, umewagawa wabunge ambapo baadhi yao wameupinga na kusema unakinzana na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeingia.
Akisoma muswada huo jana, Kabaka alisema ulitungwa kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa ajira za wageni nchini.
Alisema sheria hiyo inatarajiwa kuweka mamlaka moja itakayoratibu na kurahisisha upatikanaji wa vibali vya ajira za wageni kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji nchini na kuongeza uwajibikaji katika soko la ajira.
Mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya (CCM), aliipongeza serikali kwa kuleta mswada huo akisema utasaidia ajira kwa vijana.
Alisema pia kuwa, lazima serikali ihakikishe inaepuka watu wanaokuja kwa mwamvuli wa uwekezaji na baadaye kujiingiza kwenye biashara ndogondogo.
Akisoma maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Albert Obama, ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo alitaka itungwe sheria ndogo itakayoelekeza juu ya utoaji wa vibali.
“Mapendekezo ya kumuombea mtu kibali yatapelekwa kwenye Idara ya Uhamiaji kabla ya kufika kwa waziri kwa ajili ya utekelezaji,” yanasema mapendekezo hayo.
Kamati hiyo pia ilisema kifungu cha 5(3) kinamuelekeza kamishna wa kazi kuwa ndiye mwenye mamlaka ya kutoa vibali kwa Tanzania bara, “kifungu hiki hakijaweka muda wa kutoa vibali hivi”.
Kwa upande wake, Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Cecilia Paresso, alisema Tanzania imeingia kwenye mikataba ya kikanda ambayo inakinzana na sheria iliyowasilishwa bungeni.
Alisema mikataba hiyo ni pamoja na ule wa Ushirikiano wa Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles