24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MUSUKUMA, MADIWANI 8 KORTINI KWA KUKUSANYIKA ISIVYO HALALI

NA HARRIETH MANDARI-GEITA


MBUNGE a Geita Vijijini, Joseph Musukuma (CCM) na madiwani wanane jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita, Ushindi Swalo, wakituhumiwa kwa mashitaka manne ikiwamo kukusanyika isivyo halali.

Mengine ni kufanya mkutano bila kibali, kuziba barabara, na kufanya uharibifu wa bomba la maji.

Madiwani hao wanane wa CCM ni Stephen Werema, Costantine Mtani, Ngudungu Joseph, Martin Kwilasa, Hadija Joseph, Michael Kapaya na Maimuna Kaitila.

Mwanasheria wa Serikali, Emin Kiria akishirikiana na wakili Hezron Mwasimba alidai mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Ushindi Swalo kuwa Septemba 13 mwaka huu asubuhi, watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda makosa hayo ya jinai.

Katika shitaka la kwanza ilidaiwa kuwa Septemba 9 mwaka huu washitakiwa walikula njama kwa nia ya kutenda kosa la jinai, katika ukumbi wa mikutano wa GEDECO.

Ilidaiwa kuwa kitendo hicho ni kinyume na kifungu namba 386(1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002

Katika shitaka la pili ilidaiwa watuhumiwa Stephen Werema, Costantine Mtani, Ngudungu Joseph, Martin Kwilasa, Hadija Joseph, Michael Kapaya na Joseph Musukuma, isipokuwa Maimuna Kaitila, walifanya mkusanyiko isivyo halali kinyume na Sheria ya Makosa ya Jinai Namba 75 (1) na kifungu Namba 75, kifungu kidogo cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002.

Ilidaiwa pia kuwa mtuhumiwa wa kwanza hadi wa nane, isipokuwa Maimuna Kaitila, waliweka kizuizi katika barabara kuu inayokwenda katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kinyume cha Sheria C 239 ya Makosa ya Jinai kifungu Namba 16 cha Sheria ya Makosa ya Jinai Mwaka 2002.

Kiria alidai kuwa Septemba 14 mwaka huu 12 asubuhi katika maneo ya Mtakuja, watuhumiwa hao waliziba barabara inayokwenda mgodini humo na kusababisha wafanyakazi kushindwa kwenda kazini.

Shitaka la nne pia linawahusisha watuhumiwa wanane (isipokuwa mtuhumiwa Maimuna Mingisi).

Ilidaiwa kuwa Septemba 14 mwka huu katika Kijiji cha Nungwe wilayani Geita, watuhumiwa hao waliharibu bomba kuu la maji linalosambaza maji katika mji wa Geita.

Bomba hilo hupeleka maji hayo katika bwawa la Nyakanga linaloyasambaza kwa wakazi wa Mkoa wa Geita, uharibifu uliosababisha wananchi na mgodi wa GGM kukosa maji.

Washitakiwa hao wanaotetewa na mawakili Deo Ngangeli na Neema Christian, walikana mashtaka yote.
Waliachiwa kwa dhamana ya Sh milioni tano kila mmoja hadi Oktoba 10 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Wakati huohuo, mkutano wa majadiliano baina ya GGM na madiwani wa Halmashauri ya Mji na Halmashauri ya Wilaya ya Geita kuhusu madai ya Sh bilioni 24.6, fedha za ushuru wa huduma ambazo mgodi huo ulitakiwa kuzilipa katika miaka tisa kutoka mwaka 2004 hadi 2014, umekwama kufanyika.

Mkutano huo ambao ulipangwa kuwahusisha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Mendrad Kalemani, Kamishna wa Madini, Benjamin Mchwampaka, haukufanyika baada ya madiwani kutojitokeza wakidai baadhi yao wanahofia kukamatwa na polisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles