27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Mustafa aahidi kutokomeza zero kata ya Nguvumali

Amina Omari,Tanga

Aliyekuwa Meya wa Jiji la Tanga, Seleboss Mustafa ameahidi kuwa iwapo atachaguliwa kushika nafasi ya Udiwani atahakikisha anafuta zero katika kata yake.

Ahadi hiyo aliitoa wakati wa zoezi la kurudisha fomu ya kugombea nafasi ya Udiwani katika kata ya Nguvumali kwenye ofisi ya Msimamizi wa uchaguzi katika kata hiyo ambapo amesema kuwa atahakikisha anaondoa zero katika shule ya sekondari iliyoko katika kata hiyo.

“Nimeongoza kwa awamu tatu ambazo zote nilikuwa na vipaumbele ambavyo nimeweza kuvitekeleza hivyo awamu hii ni kusimamia ufaulu kwa wanafunzi wa shule yetu ya sekondari,” amesema Mustafa.

Amesema kuwa atahakikisha anashirikiana na wazazi wa wanafunzi katika eneo hilo kuhakikisha wanapunguza ziro kwa kusimamia masomo ya wanafunzi hao.

Aidha ameipongeza tume ya uchaguzi NEC kwa kuendesha zoezi la uchukuwaji wa fomu katika utaratibu mzuri ambao hauonyeshi upendeleo kwa Chama chochote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles