KATIBU Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye, amefurahia wingi wa mashabiki waliojitokeza kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Hawassa kushuhudia michuano hiyo.
Kutokana na hilo, Musonye amewapongeza waandaaji wa mechi za mji wa Awassa, ambapo kwa hatua iliyobakia ya michuano hiyo yataendelea katika mji wa Addis Ababa na kujipa moyo yatamalizika kwa mafanikio makubwa.
“Nina furaha kubwa kwa namna mashabiki walivyojitokeza Hawassa na nina furaha kwa sapoti wanayotupa pamoja na mwenendo wao. Idadi yao kwenye mechi ni kubwa sana tuliyoiona kwenye CECAFA kwa miaka ya hivi karibuni,” alisema.