31.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

MUSEVENI: WABAKAJI WAUAWE

KAMPALA, UGANDA

RAIS Yoweri Museveni amelaani vikali ubakaji akisema wahusika wa vitendo hivyo wanastahili kuuawa.

Museveni alitoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho ya miaka 36 ya ‘Tarehe Sita’ Viwanja vya Boma wilayani Apac juzi.

 “Mbakaji ni muuaji na kwa sababu hiyo, naye anastahili kuuawa,” alisema.

“Sababu ya UPDF (Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda) kufanikiwa ni pamoja na uwapo wa nidhamu. UDPF inaheshimu watu. Wakati unapomuua mtu, tutakuua. Iwapo wewe (askari) unambaka mwanamke, tutakupiga risasi.”

Aliendelea kusema kuwa wabakaji wanahusika na usambaaji wa maradhi hatari ya kuambukiza kwa watu wasio na hatia.

Hata hivyo, Ibara ya 22 ya Katiba ya Uganda inasema “hakuna mtu anayepaswa kudhulumiwa maisha yake isipokuwa tu kupitia adhabu ya kifo iliyopitishwa na mahakama baada ya kutiwa hatiani na adhabu hiyo kuthibitishwa na mahakama ya juu.”

Maadhimisho ya Tarehe Sita, yanamaanisha Februari 6, ambayo vuguvugu la msituni la National Resistance Army (NRA) kabla halijabadilishwa kuwa UPDF baada ya kuingia madarakani walianza mapambano ya msituni.

Katika siku hiyo mwaka 1981, wapiganaji 27 wa kundi hilo wakijihami kwa silaha chache, walivamia kambi za jeshi za Kabamba.

Huo ukawa mwanzo wa mapambano ya msituni dhidi ya utawala wa kidikteta, usio wa kikatiba na wenye kukiuka haki za binadamu.

Harakati za kundi hilo pamoja na vuguvugu lake la kisiasa la National Resistance Movement (NRM) ambalo kwa sasa ni chama tawala, zilishuhudiwa zikiingia Kampala na hatimaye kumwingiza Museveni madarakani Januari 26, 1986.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles