29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

Museveni kugombea urais 2021

KAMPALA, UGANDA

CHAMA tawala cha National Resistance Movement (NRM) nchini Uganda kimemteua Rais Yoweri Kaguta Museveni kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi wa mwaka 2021.

Hiyo ina maana ya kuwa, kiongozi huyo mwenye miaka 74, na aliyeingia madarakani kwa mtutu wa bunduki mwaka 1986, atagombea urais kwa muhula wa sita. NRM kimekubali, katika kikao kilichoongozwa na Museveni jana kuwa aendelee na urais uchaguzi utakapofanyika mwaka 2021.

Miaka ya nyuma, Museveni aliwahi kusema kuwa, viongozi ‘wanaodumu’ madarakani ndio chanzo cha matatizo barani Afrika. Hata hivyo, wakati akigombea muhula wa tano wa madaraka mwaka 2016, alisema kuwa huo haukuwa muda muafaka kwake kuondoka madarakani kwani bado alikuwa na kazi ya kufanya.

Ugombea wake katika uchaguzi ujao unakuja baada ya kusaini kuwa sheria muswada ambao uliondoa ukomo wa urais wa miaka 75. Hata hivyo, kupitishwa kwa muswada huo bungeni kuligubikwa na vurumai kubwa kutokana na kupingwa na wabunge wa upinzani.

Ilifikia mahala makonde yalirushwa ndani ya Bunge baina ya wabunge wa upinzani na maafisa usalama ambao wanaaminika ni kutoka kikosi cha ulinzi wa rais.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles