24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Murray: Dharau zimeniponza US Open

STAA wa tenesi, Andy Murray, amesema alishindwa kumuheshimu mpinzani wake, Stefanos Tsitsipas, na ndiyo maana akaambulia kichapo katika mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano ya US Open.

Katika mchezo huo uliochukua saa nne na dakika 49, Tsitsipas raia wa Ugiriki alimchapa Muingereza huyo kwa seti 2-6 7-6 (9-7) 3-6 6-3 6-4.

Anachozungumzia Murray ni kwamba aliongoza kwa seti mbili lakini alipotea kwenye reli na kisha kumruhusu Tsitsipas atawale mchezo.

Hata hivyo, Murray alionekana kumtupia lawama mpinzani wake huyo kwa kitendo chake cha kutumia dakika nane kwenda chooni. “Hata kama ningeshinda, ningelisema hilo. Naahidi kabisa,” amesema staa huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles