Timu ya Uingereza imetwaa taji hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1936, huku Murray akifanikiwa kumshinda mpinzani wake raia wa Ubelgiji, David Goffin.
Murray alimshinda mapinzani huyo kwa jumla ya seti 6-3, 7-5, 6-3 na kumfanya Goffin kupoteza kwa jumla ya seti 3-1.
Murray amejiongezea historia kubwa baada ya kutwaa mataji ya michuano ya Wimbledon, michuano ya wazi ya US Open na ile ya Olimpiki.
Mchezaji huyo amekuwa na furaha kubwa ya kulipa taifa lake ubingwa huo, huku akidai kuwa hawezi kuamini kilichotokea.
“Nina hisia kali sana na siwezi kuelezea, ninaamini itachukua muda mrefu kuweza kupungua kwa hisia hizo, maana nina furaha kubwa ambayo itaendelea maishani mwangu.
“Haikuwa kazi rahisi kuweza kushinda kwa kuwa mchezo ulikuwa mgumu, lakini kwa upande wangu ninashukuru nimefanikiwa kutwaa taji hilo na kuliwakilisha vema taifa langu,” alisema Murray.