21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

MURO AWATAKA VIJANA WASIPOTEZE MUDA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Na JANETH MUSHI-ARUMERU


MKuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, amewataka vijana wilayani hapa kujiunga katika vikundi na kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo na kuangalia fursa za kiuchumi badala ya kutumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii.

Amesema Serikali inaendelea kuboresha mazingira rafiki kwa vijana kustawi kijamii na kiuchumi huku akitolea mfano asilimia nne ya mikopo inayotolewa katika kila Halmashauri kwa ajili ya vikundi vya vijana.

Muro ameyasema hayo jana wilayani hapa mkoa wa Arusha, wakati uzinduzi wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Kimataifa ya Vijana ambapo kwa Tanzania maadhimisho hayo kitaifa yanatarajiwa kufanyika Agosti 12, wilayani hapa.

“Vijana wakijiunga katika vikundi kuna fursa nyingi zitakazowasaidia kujiinua kiuchumi na kuwa nikiwa kama msimamizi wa wilaya hii nitasimamia na kuhakiksiha mikopo hiyo inayotokana na mapato ya ndani inawafikia walengwa.

“Wiki ijayo nitakutana na watendaji wa halmashauri kuangalia vijana walionufaika na mikopo iliyotolewana wamefikia hatua gani vijana tangu wapate mikopo hiyo, kama alivyowahi kusema Rais John Magufuli, fedha ya serikali ni moto ukiigusa itakuunguza au itakubabua vivyo hivyo fedha za vijana wilayani hapa hazitaliwa,” amesema na kuongeza;

“Ila vijana msikae tu, jiungeni kwenye vikundi angalieni fursa za kufanya, tengenezeni miradi tutatafuta wadau mbalimbali wa maendeleo wawasaidie, tumieni fursa zilizopo kujiinua kiuchumi msiishie kutumia muda mwingi kwenye instagram, whatsapp na mitandao mingine ya kijamii bila kujishughulisha.”

Aidha katika uzinduzi wa maadhimisho hayo vijana kutoka mikoa mbalimbali waliungana na wadau wengine kupanda miti katika Kituo cha Polisi Tengeru na kutembelea vituo vya vijana na ┬ámiradi mbalimbali inayotekelezwa na vijana katika maeneo ya King’ori mkoani Arusha na Kwasadala mkoani Kilimanjaro.

Naye Tausi Hassan kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya idadi ya watu (UNFPA), amesema wameungana na wadau wengine na kupanda miti kutokana na ongezeko la binadamu na ongezeko la shughuli za binadamu ambazo zinaathiri mazingira, hivyo wameona wanapokutana vijana ni vema kuendeleza uoto wa asili.

“UNFPA sisi tunawalemga zaidi vijana waliopo pembezoni kwa sababu mipango mingi haiwafikii wao, tunatumia nafasi kuwafikia hivyo tunashirikiana na mashirika yanayojishughulisha na masuala ya vijana,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles