24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Munalove: niliuza gari kumuuguza mwanangu, niliowaamini walinikimbia

Anna Potinus

Mwanadada aliyejipatia umaarufu kupitia mitandao wa kijamii wa Instagram, Rose Nungu maarufu Munalove ambaye mwaka jana alifiwa na mtoto wake wa pekee Patrick baada ya kuugua kwa muda mrefu ameweka wazi story yake tangu kumuuguza hadi mtoto huyo anafariki.

Akizungumza katika mahojiano na TV ya mtandaoni, Muna amesema hakuna mtu yeyote aliyemsaidia katika kipindi alichokuwa anamuuguza mtoto wake, hali iliyosababisha kuuza gari ili kupata fedha za kumuuguza.

Amesema alipitia wakati mgumu alipokuwa akimuuguza lakini watu wote aliowaamini wamlimkimbia katika kipindi alichowahitaji zaidi.

“Watu hawajui nilihangaika kwa kiasi gani kwasababu hawajui hata Patrick alifika vipi hapa gharama gani nililipia lakini wao walikuwa wana kazi ya kunichafua tu kwenye mitandao bila kujua nilichokuwa ninapitia.

“Kuna wakati nilitamani hata kujiua au mwanangu aamke awaambie kuwa wanamsingizia mama yangu, wale wote niliokuwa ninawaamini walinikimbia nikabaki peke yangu na nilikataa kuwapa mwili hadi tulipoandikishana wakubali kwamba nilihangaika mwenyewe bila kupata msaada wa mtu yeyote.

“Hata yule aliyekuwa anadai mtoto ni wake hakukanyaga mochwari badala yake alimtuma rafiki yake, nakumbuka Casto alinitumia meseji akaniambia anaumia anaposikia maneno yaliyokuwa yanaendelea na hivyo akanitaka nikubali tu ili tumpumzishe Patrick kwa heshima,” amesema Munalove

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles