25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Mume wa mwanamke aliyetoweka akiri kumuua mkewe, kumchoma kwa mkaa magunia mawili

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mume wa mwanamke anayedaiwa kupotea kwa zaidi ya miezi miwili, Naomi Marijani (36), Khamis Luwongo (Meshack), amekiri kumuua mkewe na kisha kumchoma kwa mkaa magunia mawili na kumzika shambani kwake.

Mwanamke huyo anadaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha na picha yake kusambazwa katika mitandao ya kijamii sanjari na taarifa za kutoweka kwake.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kigamboni, Thobias Walelo mtuhumiwa huyo anayeshikiliwa na polisi kwa sasa, katika maelezo yake amedai mara baada ya mauaji hayo aliuchukua mwili wa mke wake na kuuweka kwenye shimo alilochimba kwenye banda lake la kufugia kuku.

Amedai baada ya kuuweka shimoni aliweka mkaa magunia mawili na mafuta ya taa kisha akawasha moto ulioteketeza mwili wote hadi kubaki majivu kisha alichukua majivu hayo akaweka kwenye mfuko na kubeba kwa kutumia gari lake lenye namba T206CEJ, Subaru Forester yenye rangi nyeusi na kuupeleka shambani kwake lililoko Kijiji cha Mlogolo, mkoani Pwani.

“Alichimba shimo kwenye shamba lake kisha kuweka hayo majivu, akayafukia na akapanda mgomba juu yake, kisha alikaa nyumbani kwake akisema mke wake ametoroka nyumbani Mei 15 na kufungua taarifa ya mke wake kutoroka nyumbani na kupewa RB ya kituo kidogo cha Mjimwema  MJ/RB/234/2019.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles