28 C
Dar es Salaam
Monday, January 24, 2022

MUME, MKE WATALIKIANA KUMFURAHISHA MPENZI WAO WA KIKE

WAKATI Cristina na Benno Kaiser walipokula kiapo cha ndoa yao, hawakutarajia kuwa atatokea mwanamke mwingine atakayesababisha talaka katika ndoa yao.

Cristina mke wa Benno pia ni msagaji. Miaka 12 baadaye, wazazi hao wenye watoto watatu wanajiandaa kutalikiana ili rafiki yao wa kike asipate wivu.

Sasa Cristina (31) au Benno (37) mmoja wao atamuoa mpenzi wao huyo wa kike mwenye umri wa miaka 21 ili wote watatu wawe na haki ya kisheria ya watoto wao.

Lengo pia ni kumuondoa Sierra wasiwasi wa kumwagwa siku za usoni bila haki za kisheria ukizingatia ndoa halali isingefanyika wakati tayari kuna ile kati ya wenzi hao aliowakuta.

Benno, msaidizi katika ofisi ya wanasheria alisema: “Cristina na mimi tuliamua kuwa hiki ni kitu tunachopaswa kukifanya ili Sierra afahamu kiasi gani tunampenda na kwamba tunataka awe sahemu ya familia yetu.

“Manufaa ya mmoja wetu kumuoa, zitakuwa nyingi kwa namna tofauti.

“Atatambulika kisheria kama mzazi kwa watoto na muhimu zaidi, itamuonesha kwamba hiki si kitu cha muda, sote tunampenda sana na ni kitu kinachopaswa kuwa cha kudumu.”

Cristina na  Benno walikutana 2005 wakati wote wakilitumikia jeshi la polisi la Marekani.  Walioana miezi minne baadaye na mwaka mmoja baada ya ndoa yao walibarikiwa mtoto wao wa kwanza Isaiah (11) na baadaye Rebecca (7) na Brianna (6).

Lakini baadaye Cristina, ambaye pia ni msagaji alianza kuhisi kitu fulani kikikosekana katika maisha yake ya ndoa.

Cristina, ambaye pia ni msaidizi katika asasi ya wanasheria alisema: “Awali, lilikuwa wazo langu kufungua milango ya ndoa. Nilileta kwa  Benno na kumwambia kwamba ningependa kumtambulisha katika uhusiano wetu mwanamke mwingine kuangalia namna hali itakavyoenda.

“Tulikuwa tayari tuna mengi ya kufurahisha. Watoto watatu, ndoa imara na kumuongeza Sierra katika maisha yetu kumeifanya iimarike mara mia, nahijisi kama niko kamili sasa.”

 

Cristina alikutana na Sierra katika kituo kimioja cha maduka ya kisasa mjini Las Vegas, wakaanza uhusiano wao, ambapo Sierra alikubali kujitosa katika utatu huo.

Sierra alisema: “Awali nilisita kujihusisha na uhusiano wa wenzi walio katika ndoa.”

 “Lakini wakati nilipotumia muda pamoja nao nilibaini kuwa kila kitu kiko sawa na kwamba wanachukulia kawaida na hivyo nisiwe na hofu na hivyo nikajitosa.”

Benno alisema: “Mimi, Sara na Cristina sote tunaishi kama mwili mmoja na tulipoonana mara ya kwanza sote tulifahamu fika tutakuwa naye daima.

 “Hisia zangu kwa wanawake hawa wawili zi sawa. Nawapenda wote bila ubishi. Wote ni sehemu ya maisha yangu na najihisi siwezi kutafakari maisha bila mmoja wao.”

Anaendelea kusema: “Sote tunachangia kitanda kimoja, tunachangia kila kitu, hivyo tangu tukutane na Sierra hakuna usiku ambao hatukushea uhusiano wa ndoa sisi kwa sisi.

“Daima tunakuwa bize. Kuna mikono mingi kila mahala. Uzuri wa penzi letu ni kwamba tunaishi maisha changamfu ya ndoa na salama kabisa kutokana na kupendana kwa dhati.”

Tangu ahamie katika nyumba hiyo ya familia, Sierra amekuwa mlezi mkuu wa watoto watatu, akikaa nyumbani wakati Benno na Cristina wakienda kazini.

Benno alisema: “tulizungumza na watoto wetu kabla ya hili na tulitaka wafahamu atakuwepo mzazi wa tatu katika maisha yao. Watoto wetu wamekuwa na msaada katika hili na wametuelewa sana.” 

 Sasa Sierra anasema anajihisi yu mama kwa watoto wa Cristina, na watoto hao wamethubutu kumwita mama.

Anaendelea kusema: “Najihisi kabisa kama mama yao. Nina matumaini nao wananipenda, huniita ‘mama Sara’ na ninawapenda sana.

“Sijisikii wivu kwamba watoto si wangu wa kuwazaa. Kuwapenda si lazima kwamba niwazae. Hicho si kikwazo cha kuwapenda wote.”

 Sierra anasema: “kiuhalisia hakuna wivu katika uhusiano wetu. Wakati mwingine kuna changamoto ya mawasiliano kwa sababu kuna watu watatu badala ya wawili, lakini tunaweza kuikabili.

“Daima tumekuwa katika kila hali nzuri na tunafanyia kazi matatizo yetu.”

Mwaka jana Benno na Cristina walichukua uamuzi wa kuwasilisha mpango wa kutalikiana, lakini lengo likiwa kuendelea kuishi pamoja.

Na mara talaka itakapotolewa baadaye mwaka huu Benno au Christina mmoja wao atamuoa Sierra, ijapokuwa hawajaamua nani miongoni mwao atakayemuoa.

Sierra alisema: “Ni wazo la Benno na Christina kutalikiana, lakini hilo halitabadili kitu katika uhusiano wetu watatu, itahusu nani kamuoa nani kisheria!.

“Waliamua kwamba badala yao wao kuonekana ndiyo halali kisheria, ili kunitoa wasiwasi kuwa watakuja nimwaga huko mbele na kukosa stahili zangu, watengane ili kutoa nafasi mmoja wao kunioa – nawapenda wote.”

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
176,415FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles