25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Mukoba ang’aka walimu kulazimishwa kushona sare  

waziri-wa-elimu-dr-joyce-ndalichakoNA HARRIETH MANDARI

RAIS wa Chama cha Wafanyakazi  (TUCTA) na Chama cha Walimu (CWT), Gratian  Mukoba, amesema ni kinyume cha sheria kuwalazimisha walimu kushona sare za mwenge au sherehe yoyote.

Kauli hiyo ya Mukoba imekuja wakati ambako kuna barua inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii iliyotolewa na Halmashauri ya Mji wa Shinyanga  kwenda kwa  mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Nyashimri, ikiwataka walimu kushona sare za sherehe ya mwenge wa uhuru.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi kuhusiana na barua hiyo, Mukoba alisema kushona sare yoyote ni hiari ya mtu.

“Jambo hilo si sahihi na halipo kabisa na ni kinyume cha sheria na kanuni, ni sawasawa na kuwaambia walimu kwamba kuna harusi wanatakiwa washone sare ya harusi na iwapo hawana pesa watakopeshwa, watakopeshwa kwa nini na kwa kwa riba gani, hilo  halikubaliki,” alisema Mukoba.

Alisema hata anayewakopesha anakiuka sheria na hana nia njema na walimu na kwamba anataka kuwaibia hela zao kwa sababu mwisho wa siku atakuja kuwakata mshahara pesa nyingi.

Katika barua hiyo yenye kichwa cha habari ‘Sare ya mwenge wa uhuru kwa kila mtumishi’ ambayo aliandikiwa mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Nyashimbi, unalazimisha walimu kushona sare hiyo na pia kuhudhuria sherehe hizo.

“Sare imeshachaguliwa, ni kitenge na kinapatikana katika ofisi ya ugavi ya halmashauri ya mji iliyopo Kadeko kwa shilingi 30,000 kwa vipande vitatu na wafanyakazi ambao hawatakuwa na pesa mkononi watakopeshwa na mkurugenzi wa mji na atawakata kwenye mishahara yao kwa awamu mbili, yaani kila mwezi shilingi 15,000,” ilisema barua hiyo.

Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Kahama, Deogratius Kapami, tarehe ya mwisho kwa mtumishi wa halmashauri kununua sare hiyo ni Septemba 28, mwaka huu na kwamba wanaweza kununua kipande kimoja kwa Sh 10,000, lakini hakitakopeshwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,436FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles