29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mukandala ataka marekebisho mfumo wa siasa nchini

Andrew Msechu, Dar es Salaam



Aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Rwekaza Mukandala amesema mfumo wa vyama vingi ulioanzishwa rasmi nchini mwaka 1992, ulikuja kwa shinikizo kutoka nchi tajiri na Mfuko wa Fedha wa Dunia (IMF) ambapo sheria zilizowekwa ziliakisi mazingira ya wakati huo.

Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa jijini Dar es Salaam leo Jumatano Septemba 19, Profesa Mukandala amesema sera za kiuchumi zilizopokelewa wakati huo ikiwamo ubinafsishaji wa vyanzo vya uchumi tayari zimeshafanyiwa mabadiliko baada ya kuona haziendani na uhalisia, hivyo ni vyema pia kuangalia katika mfumo wa siasa.

“Lakini pia iko haja ya kufanya marekebisho katika mfumo wa siasa nchini, ili kuwezesha siasa zenye ushindani lakini mabadiliko hayo lakini yawe katika hali isiyoathiri shughuli za kila siku za maendeleo ya watu,” amesema.

Akifafanua, Profesa Mukandala amesema katika hali iliyopo nchini kwa sasa, mabadiliko hayo ni muhimu kwa kuwa sheria zinazosimamia mfumo wa kisiasa uliopo umeundwa miaka zaidi ya miaka 20 iliyopita na kwa sasa hauakisi mabadiliko ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

“Tunaona tangu kuingia katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi unaohitaji ushindani, siasa za kiliberali zimekuwa na athari katika nchi zetu. Tunahitaji ushindani uwepo, japokuwa usiozidi mipaka na kuhatarisha amani,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles