22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

MUHONGO ATAKA BILI ZA UMEME ZILIPIWE TANESCO

Na Veronica Simba – Singida


WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amewataka wananchi wanaounganishiwa huduma ya umeme vijijini, kufanya malipo katika Ofisi za Tanesco na si vinginevyo.

Aliyasema hayo hivi karibuni katika Kijiji cha Mkwese, Wilaya ya Manyoni mkoani Singida wakati akizindua Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) mkoani humo.

Profesa Muhongo alisema wananchi wengi wamekuwa wakitapeliwa na watu mbalimbali kwa kuombwa rushwa ili waunganishiwe umeme au kulipishwa gharama zaidi ya zile zinazostahili.

Alisema baada ya kufuatilia, imebainika wanaofanya utapeli huo ni watu wasiohusika kabisa na uunganishaji umeme.

Aliitaka Tanesco kuhakikisha inaendelea na kazi ya kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma zote wanazotoa ili wanan1`chi wawe na uelewa wa kutosha.

Alisema: “Baadhi ya wananchi wanadhani REA ndio wenye jukumu la kuchukua malipo kutoka kwa wananchi wanaounganishiwa umeme vijijini.

“Anayepokea malipo yote ya umeme ni Tanesco na si REA wala wizara, wananchi mjue hilo. Mwingine yeyote akidai malipo ya umeme, mkatalieni,” alisisitiza.

Aidha, Waziri Muhongo alitoa rai kwa Serikali za Vijiji kutoa ushirikiano kwa Tanesco, ikiwezekana kuwapatia chumba au ofisi ya kutolea huduma kwa siku watakazopanga kutoa huduma katika vijiji husika.

Waziri Muhongo alieleza kuwa, Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu mkoani Singida utatekelezwa kwa vipindi viwili tofauti, ambapo sehemu ya kwanza itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 185 kwa gharama ya Sh bilioni 47.36.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,220FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles