25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Muhimbili waunda mavazi ya wataalam Wa afya watakaohudumia wenye corona

Na AVELINE KITOMARY, DAR ES SALAAM 

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili, imeshona vazi maalumu (coverall) ambalo ni sehemu ya mavazi ya watoa huduma (PPE) ili kujikinga wakati wanapotoa huduma kwa wagonjwa watakaobainika kuambukizwa virusi vya  corona (COVID 19).

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es salaam,  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Hospitali hiyo, Dk Hedwiga Swai alisema jitihada hizo ni sehemu katika kuunga mkono kauli ya Rais Dk John Magufuli, kwamba Watanzania wanaweza na sio lazima kila kitu kitoke nje kwani malighafi zilizotumika zote zinapatikana katika viwanda vilivyopo nchini.

Alisema PPE zinazotoka nje ya nchi hugharimu fedha nyingi za Tanzania ambapo vazi moja ni kati ya Sh  350,000 hadi Sh 500,000 huku  ikitegemea huku iliyoshonwa Muhimbili ikigharimu Sh 30,000. 

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Hospitali hiyo, Dk Hedwiga Swai

“Tumeamua kushona vazi hilo ambalo linakaribiana na viwango vya WHO (Shirika la Afya Duniani) na si kama watoa huduma tulioko msitari wa mbele kuwahudumia, tumeridhika kuwa vazi hili linakidhi viwango na mahitaji yetu hapa nchini” alieleza  Dk Swai.

Alisema katika kukabiliana na changamoto ya kutokapatikana kwa urahisi mavazi haya, Muhimbili ina wajibu wa kutoa mwelekeo, ubunifu wa namna ya kutoa huduma nchini na hii ni sehemu ya wajibu huo.

 “Tunatoa wito kwamba sasa viwanda vya ushonaji vinaweza kuja kupata sampuli ya aina ya vazi na malighafi zinazotumika ili bidhaa hii iweze kuzalishwa kwa wingi na kupatikana kwa gharama nafuu zaidi,”alibainisha.

Alisema hospitali ya Muhimbili inaipongeza Serikali kwa jitihada inazofanya na hatua mbalimbali zinazochukuliwa katika kukabiliana na ugonjwa huu ambao umeingia nchini nasi tunaendelea kushirikiana katika mapambano hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles