25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Muhimbili, MOI, MUHAS wachukua tahadhari dhidi ya corona

Aveline kitomary

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Aminieli Aligaeshi amesema hospitali hiyo kwa kushirikia na Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), inachukua tahadhari ya virusi vya corona kwa kuhakikisha kila mmoja ananawa mikono kabla ya kuingia ndani ya hospitali hiyo.

Aligaeshi amesema hatua nyingine iliyochukuliwa ni kupunguza idadi ya ndugu jamaa na marafiki ambao wanaenda kuona wagonjwa ambapo kwa sasa ni ndugu wawili tu wataruhusiwa kumuona mgonjwa.

“Tunawataka wafanyakazi, ndugu na jamaa wa wagonjwa wote wanaoingia eneo la Muhimbili kunawa mikono kwa kutumia maji yenye dawa yaliyowekwa katika maeneo mbalimbli ya taasisi hizo kabla na baada ya kuingia ndani ya Hospitali, wodini na sehemu za kutolea huduma.

“Tumeunda kikosi kazi kinachoratibu zoezi zima la tahadhari dhidi ya Corona ambacho kinatoa mafunzo kwa wafanyakazi wote wa taasisi hizo, wanafunzi, mafunzo kwa wakufunzi (ToT) watakaosaidia kuelimisha umma kwa kushirikiana na Wizara ya Afya.

“Uongozi wa Taasisi hizi umekubaliana kwa kauli moja kuwa kuanzia sasa wataruhusiwa ndugu wawili tu kwa kila mgonjwa mmoja wakati wa asubuhi na jioni ambapo mchana ni mtu mmoja tu atakayeruhusiwa kupeleka chakula kwa mgonjwa ili kupunguza msongamano mkubwa uliopo eneo la Muhimbili,” amesema Aligaeshi.

Hata hivyo amewaomba wananchi kuwaunga mkono ili kuongeza tahadhari zaidi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles