24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Muhimbili kuanza kupandikiza figo

Profesa Lawrence MuseruNa Veronica Romwald, Dar es Salaam

HOSPITALI ya Taifa Muhimbi (MNH) imetangaza mkakati wa  kuanzisha huduma ya kupandikiza figo.

Imesema   mpango huo utasadia  kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda nje kwa ajili ya kupata huduma ya upandikizaji wa figo.

Akizungumza na waandishi wa habari   Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Profesa Lawrence Museru, alisema  hatua hiyo  itatokana na uwezo wa kuwa na mashine 23 hadi 50 pamoja na kuongeza wataalamu.

“Katika mipango ya muda mfupi na mrefu hospitali imedhamiria kupunguza wagonjwa wanaokwenda nje kupata huduma za upandikizaji wa figo na  ifikapo mwishoni mwa mwaka huu tutaweza kupandikiza figo hapa hapa nchini.

“Si hilo tu pia tutapanua huduma za kusafisha figo kutoka uwezo wa kuwa na mashine 23  mpaka kufikia mashine 50 na pia kuongeza shifti za kuchuja figo kutoka mbili za sasa hadi kufikia tatu na pia kuchuja figo za wale wenye maambukizi ya Ukwimi na Hepatitis,” alisema Profesa Mseru.

Hata hivyo, alisema Muhimbili inakabiliwa na uhaba wa madaktari bingwa  na wauguzi   kuweza kukidhi mahitaji ya kuwahudumia wateja kwa ufanisi.

Alisema hospitali hiyo pia inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya kutolea huduma kwa wagonjwa mahututi (ICU) ambako bado inatumiwa wodi moja yenye vitanda sita pekee.

“Tunapokea wagonjwa wengi lakini tuna madaktari wapatao 300… hawatoshi ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa wanaofika hapa kila siku kupatiwa matibabu huku tukiwa na idadi ndogo ya wauguzi pia.

“Hospitali kubwa kama hii ya Muhimbili inapaswa iwe na vitanda vipatavyo 130 vya chumba cha ICU, lakini hapa tunavyo sita na tuna wodi mbili,” alisema.

Alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo ya uhaba wa vitanda vya ICU, hospitali imejipanga kufungua wodi mpya itakayokuwa na vitanda 15.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles