24.6 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

MUHAS YAZINDUA KITABU CHA MAFUNZO YA SHAHADA UDAKTARI

Veronica Romwald, Dar es Salaam

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), kimezindua kitabu kitakachotumiwa na wanafunzi wa ngazi ya shahada ya kwanza ya udaktari wa binadamu kwa ajili ya kuongeza ujuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, katika hafla fupi ya uzinduzi wa kitabu hicho, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri, Profesa Andrea Pambe, amesema kitawasaidia wanafunzi kuongeza ushindani wa utendaji wa kazi watakapomaliza masomo yao.

Profesa Pambe amesema kitabu hicho kiitwacho ‘Basic Principles of Emergency Medicine’ kinahusu matibabu ya dharura hasa kwenye idara ya magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

“Tutahakikisha kinatumiwa kwa wanafunzi wanaosomea udaktari waliopo mwaka wa nne kwani dhumuni letu wawe na skills (ujuzi) wa kutosha pindi watakapohitimu mafunzo yao,” amesema Profesa Pambe.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Tiba ya Dharura chuoni hapo ambaye ni mtunzi wa kitabu hicho Dr. Henry Sawe, amesema dhumuni la kutunga kitabu hicho limetokana na kusoma vitabu vya nje ambavyo havizingatii mazingira ya Tanzania.

“Vitabu vingi vya masomo ya udaktari tunavyotumia vinatoka nchi za nje ambazo zimeendelea havina uhusiano na mazingira ya nchi yetu, hiki kimezingatia mtaala mzima wa fani ya udaktari, vifaa tiba na aina ya madaktari waliopo nchini.

“Ni kitabu ambacho kinakidhi mahitaji kwa Watanzania ambapo hata kwa wanafunzi watakipata kwa gharama nafuu  ukilinganisha na vitabu vingine hasa vinavyotoka nje ya nchi gharama zake ni kubwa,” amesema daktari huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles