MUGHWIRA AAGIZA MWALIMU MKUU KIBOHEHE KUKAMATWA

0
752

 

Na Omary Mlekwa, Kilimanjaro

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mughwira ameagiza kukamatwa kwa msimamizi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Kibohehe, iliyopo wilayani Hai, mkoani humo na aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kutokana na kuanguka kwa ukuta wa shule hiyo uliotokana na ujenzi wa chini ya kiwango.

Aidha, serikali imeifunga shule hiyo kwa muda usiojulikana ili kupisha ukarabati wa shule hiyo baada ya baadhi ya miundombinu yake kuharibiwa vibaya na mvua hiyo.

Hatua hiyo inatokana na kuanguka kwa ukuta wa shule hiyo baada ya kunyesha mvua kali iliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa darasa la sita na kujeruhi wengine watano katika shule hiyo.

“Licha ya kufungwa kwa shule hii pia ujenzi wake ulijengwa chini ya kiwango na bila kufuata utaratibu za ujenzi hivyo basi naagiza msimamizi na mwalimu mkuu wa wakati huo shule inajengwa, wakamatwe,” amesema.

Mkuu huyo wa Mkoa ametembelea shule hiyo leo kujionea miundombinu yake baada ya mvua hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here