MUGABE YUPO SINGAPORE KWA MATIBABU

0
722

Harare, Zimbabwe


RAIS wa Zimbambwe, Robert Mugabe yupo nchini Singapore kwa matibabu ikiwa ni  mara yake ya tatu.

Mugabe ambaye ni rais mwenye umri kubwa Afrika akiwa na miaka 93, mwezi Mei mwaka huu alikuwepo Singapore kwa ajili ya matibabu ya matatizo ya macho, kwa mujibu wa msemaji wake, George Charamba.

Gazeti la The Standard linasema kuwa rais huyo ameondoka nchini humo Ijumaa iliyopita kwa matibabu kwa maelezo ya Waziri wa Habari wa Zimbambwe, Chris Mushohwe ambaye aliliambia gazeti hilo, lakini alikata kuthibitisha sababu ya safari yake nchini Singapore.

Chama tawala nchini humo cha ZANU-PF kilisema kuwa kilisitisha mkutano wa vijana ambao alitakiwa kuhudhulia  kwa sababu rais huyo atakuwa nje ya nchi.

Hata hivyo, Charamba na Mushohwe hawa kupokea simu au kujibu ujumbe mfupi wa maneno kwa ufafanuzi zaidi.

Licha ya kuongezeka kwa wasiwasi juu ya afya yake, Mugabe amefanya safari  za nje 10  kwa mwaka huu na ametangaza kugombea tena katika uchaguzi wa mwaka 2018.

Mugabe ametawala Zimbabwe tangu nchi hiyo ilipopata uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka1980.

Mugabe amesafiri maili 200,000 akiwa angani tangu mwanzoni mwa 2016 ambapo ametumia Dola za Marekani milioni 53  kwa safari za nje mwaka jana ambacho ni zaidi ya mara mbili ya bajeti ya awali ya Dola milioni 23 kwa mujibu wa takwimu za serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here