24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mufuruki aachia ngazi Bodi Vodacom

Grace Shitundu

Mfanyabiashara maarufu nchini, Ali Mufuruki ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Vodacom ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo kuanzia Desemba mosi mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na kusainiwa na Katibu wa kampuni, Caroline Mduma, ilieleza kwamba Mufuruki alifikia hatua hiyo ili kupata muda zaidi wa kuweza kuendeleza biashara zake.

Pia taarifa hiyo ilieleza kuwa Mufuruki ametangaza kujiuzuru nafasi za mkurugenzi huru na kamati ya uteuzi wa kampuni.

Mfanyabiashara huyo ambaye pia Ofisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya Infotech Investmen Group amedumu katika bodi ya Vodacom kwa muda wa miaka miwili tangu alipoingia Agosti mosi mwaka 2017.

“Katika muda wote wa uongozi wake Mufuruki ametoa mchango mkubwa kwa kampuni na uongozi wake, bodi inachukua nafasi hiyo kumshukuru kwa mchango wake huo na uongozi wake” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo bodi ipo katika mchakato wa kupata mkurugenzi huru mwingine atakayechukua nafasi ya Mufuruki.

MUFURUKI NI NANI?

Wakati fulani Mufuruki alipofanya mahojiano na gazeti dada la hili la RAI, alipoulizwa Mufuruki ni nani? Alijibu;  “Mimi ni Mtanzania wa kawaida”.

Pamoja na hayo, Mufuruki ni mmoja wa matajiri ambao kwa mujibu wa majarida maarufu ya masuala ya uchumi duniani, Forbes na Ventures Africa yanautaja utajiri wake kuwa unatokana na biashara mbalimbali za rejareja na za ushirika.

Mufuruki ni Mwenyekiti wa Jukwaa la wakurugenzi watendaji wa makampuni mbalimbali nchini (CEOrt),  mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Tanzania Infotech Investiment Group. Kampuni hiyo inajumuisha Watanzania na Waganda kwa ajili ya kuuza bidhaa za Afrika kusini za Woolworth. Infortech hufanya kazi ya uendelezaji makazi na ukodishaji, matangazo na shughuli za mawasiliano.

Novemba mwaka 2012 alitajwa na Jarida la Ventures Africa kuwa mmoja wa wafanyabiashara watano ambao nui matajiri zaidi nchini. Mbali na Mafuruki wengine ni Said Bakhresa, Gulam Dewji, Rostam Azizi na marehemu Reginald Mengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles