23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

Mufti wa Tanzania awataka Waislamu kumuombea Rais Samia

Na Seif Takaza, Singida

Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi, amewataka waumini  wa Dini ya Kiislamu nchini kumuombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ili aweze kuliongoza Taifa kwa amani na utulivu.

Mufti ametoa wito huo jana alipokuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya 17 ya Elimu Maarufu ( Nnujuum Day) yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho mjini Singida.

Mufti Zuberi alisema ni jukumu la Waislamu na Waumini wa dini zingine kumuombea Rais wetu Mama Samia Suluhu  Hassan baada ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa  awamu ya tano  Hayati Dk. John  Magufuli kilichotokea Machi 17, jijini Dar es Salaam.

“Ndugu zangu Waislamu natoa wito kwa Waislamu wote  na jamii  kwa ujumla tumuombee dua Rais wetu wa Jamhuriya ya Muungno wa  Tanzania  Mama Samia Suluhu Hasasan ili Mwenyezi Mungu aweze kumpa nguvu za kuliongoza taifa hili ili liwe na amani na utulivu,” alisema Mufti.

Aidha, Muft Zuberi katika hafla hiyo alimpongeza Mkuu wa Chuo cha Nnujuum, Sheikh Salim Chima  kwa jithada zake za kuanzisha Chuo hicho chenya maadili ya Dini ya Kiislamu ambacho ni mfano wa kuigwa na viongozi wa dini nchini hususa viongozi wa BAKWATA.

“Natoa wito tena kwa Waislamu kushirikiana na katika mambo ya dini kuujenga Uislamu na kuachana na migogoro isiyokuwa na msingi kwani sisi Waislamu ni wamoja na alitilia mkazo kauli mbiu yake ya ‘JITAMBUE, BADILIKA, ACHA MAZOEA’.

Katika hafla hii naahidi kukisaidia Chuo hiki kwa hali na mali na nakuagiza Sheikh Issah Simba, Sheikh wa Wilaya hii kuhakikisha Chuo hiki kinasajiliwa kwa mujibuwa sheria,” amesema Mufti.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Sheikh Salim Chima alisema Chuo hicho kilianzishwa mwaka 2004 na hadi sasa kina wanafunzi 203 amba wapo katika  mafunzo ya fani mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles