28.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mufti asikitishwa kuungua shule za kiislamu

Salome Bruno na Nasra Hussein -Dar es salaam

MUFTI wa Tanzania, Sheikh Abubakari Zuberi, ameeleza kusikitishwa kwake na vitendo vya kuungua kwa shule za Kiislamu kwa siku za karibuni.

Alisema hayo kufuatia tukio la kuteketea kwa moto bweni la wavulana katika Shule ya Msingi Byamungu Islamic, iliyopo Kyerwa mkoani Kagera na kusababisha vifo vya wanafunzi 10 na wengine sita wakijeruhiwa.

Tukio hilo lilitokea Septemba 14 katika bweni la wavulana lililokuwa na wanafunzi 74, na bado chanzo cha moto huo hakijajulikana.

Alitoa pole kwa Watanzania pamoja na mkuu wa shule hiyo, Seleman Abdul, wazazi waliopoteza watoto na majeruhi katika janga hilo na wote walioguswa na kuwaombea walio hospitali.

Mufti alisema kutokana na tukio hilo, bado wanasubiri ripoti ya kamati ya uchunguzi wa moto kwenye shule za kiislamu iliyoagizwa kuundwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

 “Kutokana na mfululizo wa matukio ya kuungua shule, natoa maelekezo kwa wamiliki kuimarisha ulinzi ndani ya shule na kuchukua tahadhari kwa kina, aidha waimarishe miundombinu ya mashule ikiwemo mifumo ya umeme, shule kuwa na uzio na vifaa vya zimamoto,” alisema Mufti.

Alisema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) linaendelea kusubiri taarifa rasmi ya vyombo vya usalama kuhusu matukio haya.

Mufti aliwaasa na kuwaomba Waislamu wote na wananchi kwa ujumla kuwa na subira katika kipindi hiki na kuendelea kuilea amani iliyopo nchini.

Pia aliomba wazazi wasisite kuwapeleka watoto shule kutokana na janga hilo, kwani walimu wameshatengeneza utaratibu mzuri katika kipindi hiki.

Mufti alisema ipo tume maalumu ya uchunguzi iliyoundwa naa Waziri Mkuu Majaliwa na Bakwata, kufuatilia matukio ya moto ambayo kwa sasa yamezikumba takribani ni shule saba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles