26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Mufti apiga marufuku madufu moto

FARAJA MASINDE -DAR ES SALAAM

BARAZA Kuu la Waslamu Tanzania (Bakwata) limepiga marufuku matukio ya muziki moto au maarufu kama magoma moto yanayorasimishwa na kaswida yanayotumiwa na Waislamu katika matukio mbalimbali zikiwamo sherehe kwa kuwa yanachafua taswira nzima ya dini hiyo.

Marufuku hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir.

Alisema jambo hilo limekiuka maadili ya Uislamu na liko nje ya dini hiyo.

“Nachukua fursa hii kuwatangazia juu ya tukio ambalo limejitokeza la muziki moto ambao unarasmishwa na kaswida zinazotumika katika Uislamu ambazo zinatumika zaidi kwenye harusi… jambo hilo limekiuka maadili ya Uislamu na liko nje ya misingi ya Uislamu.

“Tunawapiga marufuku na kuwazuilia wale wote wenye kupiga kaswida hizo na muziki huu unaorasimishwa na Uislamu kwa kuwa unachafua taswira nzima ya Uislamu, maadili na malezi mema kwa watoto wetu,” alisema Mufti.

Kutokana na hali hiyo, aliwaagiza masheikh wote wa mikoa kuhakikisha wanakemea aina hiyo ya kaswida.

“Masheikh wa mikoa, wilaya na kata, nawapa agizo la kuzuia na kukemea miziki hii ambayo inachafua maadili, wakemee katika nafasi walizonazo, ikiwa ni katika misikiti, hotuba zao na mihadhara mbalimbali wanayoifanya.

“Pia nawaagiza maimamu na masheikh wa taasisi mbalimbali kukemea jambo hili na kuondosha hali hii. Mtume anasema ‘aonae jambo bovu basi aligeuze kwa mkono wake’ kila mmoja ana wajibu wa kulifanya jambo hili,” alisema Mufti.

Alisema baraza limezuia jambo hilo na iwapo atatokea mtu akaamua kufanya kwa sura na kwa picha na kwa kuegemea katika Uislamu, atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Mufti aliwaasa kina mama kuwalea vijana katika malezi yaliyo bora pamoja na kupiga marufuku kuruhusu ngoma hizo kuja kwenye sherehe za watoto wao.

“Ngoma moto hizo ambazo nimeonyeshwa na masheikh hazifai hata kidogo, siyo Uislamu, hatutaki kabisa kuona katika nchi yetu, ni mambo ya aibu, nchi yetu inahitaji watu wenye nidhamu, maadili, wasomi na viongozi wazuri wa hapo baadaye, hauwezi kupata viongozi kwa kuruhusu mambo ya namna hii yaendelee.

“Mkoa unaoongoza kwa matukio haya sasa ni Dar es Salaam, tayari baadhi ya wahusika wameanza kutiwa nguvuni maeneo ya Kigamboni,” alisema Mufti.

Alisema baraza hilo sasa litakuwa likiadhimisha Siku ya Bakwata (Bakwata Day) kila ifikapo Desemba 17 ya kila mwaka na mwaka huu, sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika viwanja vya Karimjee na kuwataka Watanzania wengi zaidi kujitokeza.

Akizungumzia miaka 58 ya Uhuru, Mufti alisema ni wajibu wa kila mmoja kufanya kazi kwa bidii huku akienzi juhudi kubwa zilizofanywa na waasisi wa taifa, ikiwamo kudumisha amani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,663FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles