29.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Mudhihir ataka wakulima kurejesha imani kwenye vyama vya ushirika

Na Mwandishi wetu-Pwani

KAMISHNA wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Mudhihir Mudhihir, amewataka wakulima kote nchini kujiunga na kujenga imani na vyama vya ushirika ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kupanga bei ya mazao kwenye soko na kuondoa unyonyaji unaofanywa na wafanyabiashara.

Mudhihir alitoa wito huo juzi wakati wa mkutano mkuu maalum wa wanachama wa Chama cha Ushirika cha Mkuranga AMCOS, kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.

Mkutano huo ulitishwa na kusimamiwa na Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Pwani, Angela Nalimi, baada ya kuibuka kwa malalamiko ya wanachama na wakulima waliokusanya korosho kwenye chama hicho. 

“Kila mkulima anautaka ushirika lakini wakiangalia unakokwenda wanakatishwa tamaa, sisi tume ya ushirika, tumeamua kuusimsmia ushirika kwa mabadilko makubwa tunayoyaleta ili urudie nguvu yake ya zamani na ushirika usiwe sehemu ya upigaji, wakulima wasiogope kujiunga na ushirika,” alisema Mudhihir.

Aliwataka viongozi wa ushirika wanaochaguliwa katika vyama vya ushirika kuwasikiliza wanachama,  kuwa waadilfu na kuongoza kwa kufuata Sheria ya Vyama vya Ushirika Namba 6 ya mwaka 2013 na kanununi zake za mwaka 2015.  

 Katika mkutano huo, wanachama wamewaondoa madarakani viongozi wa bodi na menejimenti ya chama hicho baada ya kutokuwa na imani nao kutokana na kutowasilisha baadhi ya majina kwa ajili ya malipo yao ya korosho.

Pamoja na kuondolewa madarakani, bodi ya chama cha ushirika Mkuranga AMCOS na meneja wa chama  hicho, wametakiwa kuwajibika kwa  kulipa hasara ya  Sh  18,239,760 waliyokisababishia chama hicho. 

Taarifa ya bodi hiyo ilisema, viongozi hao wamewajibishwa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Namba 6 ya mwaka 2013 kifungu cha 95 na 126 na kanununi zake za mwaka 2015.  

Mkutano huo ulitanguliwa na mkutano wa wakulima waliouza korosho kwenye  chama cha ushirika cha Mkuranga AMCOS ulioongozwa na Ofisa Tarafa wa Mkuranga, Clemence Muya aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,  Filbeto Sanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,905FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles