23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MUBENGA: LULU DIVA NI MTU SAFI, ACHA TUPIGE KAZI

NA JOHANES RESPICHIUS

MAFANIKIO msanii yoyote yule yanakuja pale ambapo nyuma yake kunakuwa na watu makini wanaoifahamu vyema biashara ya sanaa anayoifanya msanii husika, iwe filamu hata muziki.

Hata msanii awe na umaarufu mkubwa kiasi gani, pale anapokosa menejimenti basi mafanikio na umaarufu wa staa huyo hupungua kwani kazi zake hazitakwenda vile zilivyokuwa zinakwenda mwanzoni.

Hapo ndipo nafasi ya meneja inapoingia na kuchukua nafasi kubwa kwenye mafanikio ya mastaa wengi tunaowasikia wakitamba kwenye anga la muziki huko duniani, Afrika na hata nyumbani Tanzania.

Mameneja waliojizolea umaarufu na mafanikio makubwa hapa Bongo ni Babu Tale, Sallam Sk, Seven Mosha, Mkubwa Fella na Mbarouk Issa (Mubenga) kwa kuwataja wachache.

Wiki hii Swaggaz lipo na Mubenga ambaye alianza kufanya kazi zake ndani ya bendi ya TID iitwayo Top Band na baadaye akawa meneja wa Ommy Dimpoz, ambaye ni miongoni mwa nyota wakubwa wa Bongo Fleva.

Hivi sasa ameanzisha lebo inayoitwa Bangerz Entertainment na tayari ameanza kusimamia wasanii. Kuna msanii mpya anaitwa Sosy, huku kwa mara ya kwanza akimtambulisha video vixen maarufu Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ kama mmoja ya vichwa vilivyosainiwa na lebo hiyo.

KWANINI LULU DIVA?

Mubenga anasema baada ya Lulu Diva kuomba asimamiwe kazi zake, alimpa masharti na vigezo ambavyo anatakiwa avifanye.

Alimwambia ni lazima aache kushiriki kwenye skendo kwa sababu hazijengi na nguvu zote zielekezwe kwenye kazi ya muziki.

 “Isije kufika siku nikasikia kuwa Lulu amefumaniwa na mume wa mtu, maana atakayepewa lawama si yeye, bali ni meneja wake, jambo litakalotuharibia kazi, lakini hatukuwa na haraka ya kumtambulisha Lulu ili kumpima kama yupo makini na anachotaka kukifanya.

“Baada ya kujiridhisha kwamba anataka kufanya muziki na si vinginevyo, nilimpa nafasi, hivyo nitafanya kwa kadiri ya uwezo wangu ili afike anapotaka,” anasema.

Anasema lengo la  lebo ya Bangerz ni kusaidia wasanii wachanga ‘from zero to hero’ na kwamba anaamini hilo kwa wasanii aliokwisha kuwatambulisha na wale ambao bado hawajatambulishwa.

ISHU YAKE NA OMMY DIMPOZ

Anasema jambo alilojifunza baada ya kuachana na Ommy Dimpoz, ni kwamba vijana wengi wanapoanza muziki huwa na nidhamu ya hali ya juu, lakini baada ya kupata jina wanajisahau.

“Wanapoweza kukutana na mawaziri hadi rais, basi meneja anakuwa hana ishu tena na isitoshe kulingana na nilivyolelewa na imani niliyonayo nilifanya kazi na Ommy kiujamaa kwani ni rafiki yangu mkubwa tangu tupo Top Band.

“Nilipoachana na bendi, alinifuata akaniambia hawezi kubaki kule kwa sababu kuna vitu vingi  tulikuwa tumeshavifanya akibaki hawezi kuvifanya nikakubali. Kwa kuwa nilikuwa nimeshapata chaneli na watu wa vyombo vya habari ndivyo nilitumia nafasi hiyo kumsaidia.

“Nimemsimamia Ommy tangu anatoa wimbo wake wa kwanza wa ‘Nai Nai’ mpaka ‘Usiende Mbali’ alioshirikishwa na Nedy Music kwa kuwa kulikuwa na baadhi ya mambo hayaendi sawa, nilimwita kwenye kikao nikamwambia kuwa nataka nipumzike kufanya kazi kama meneja bila tatizo lolote ikawa hivyo,” anasema.

LULU DIVA AFUNGUKA

Baada ya kufanya vyema na wimbo wake wa kwanza unaoitwa ‘Milele’ aliomshirikisha Barnaba Classic, Lulu Diva, anasema kuwa wimbo huo umeweza kumtambulisha na Watanzania wameanza kuona uwezo wake.

“Milele ilipata mapokezi makubwa hasa ukilinganisha ndiyo wimbo wangu wa kwanza na ndani ya muda mfupi video ilitazamwa na watu laki 5 na zaidi wakati kuna wasanii wakongwe hawajawahi kufikisha idadi hiyo,” anasema Lulu.

UJIO MPYA CHINI YA BANGERZ

Hivi sasa Lulu Diva yupo chini ya meneja Mubenga na tayari ameingia studio kukamilisha moja ya kazi bomba kabisa inayoitwa ‘Usimuache’ akiwa amefanya peke yake ili kuonyesha uwezo katika Bongo Fleva.

“Kuna watu walisema Milele nilibebwa na Barnaba sasa Usimuache, nimefanya peke yangu ili kuionyesha jamii kuwa naweza kusimama peke yangu,” anasema.

U- VIDEO VIXEV VIPI?

Lulu Diva anasema alifanya kazi ya kupendezesha video za wasanii wa Bongo Fleva kwa malengo na lengo lake limeshatimia, hivyo hana mpango tena wa kuendelea kuwa video vixen kwa sasa.

“Nilishawahi kufanya filamu nikaacha nikaangukia kwenye u-video vixen, nao naacha kwa sababu nilifanya nikiwa na lengo la kupata kitu fulani, muda mwingi kwa sasa nitatumia kwenye muziki,” anasema Lulu Diva.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles