25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mtumishi wa Afya Tabora aliyebaka mwanafunzi afutwa kazi

Na Allan Vicent,Tabora

Babaraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Tabora limeazimia kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa Muuguzi wa Zahanati ya Kalunde, Elipidius Kweyamba, baada ya kupatikana na hatia ya kubaka mwanafunzi na kumpa mimba.

Akitangaza maamuzi ya Kamati ya nidhamu katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika leo Alhamis, Machi 11, 2021, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Ramadhan Kapela, amesema wamefikia hatua hiyo baada ya mtumishi huyo kupatikana na hatia ya kubaka hivyo kuhukumiwa na mahakama miaka 30 jela.

Amesema hukumu hiyo ilitolewa Septemba mwaka jana baada ya mtumishi huyo kupatikana na hatia ya kumwingilia kimapenzi kwa nguvu mwanafunzi na kumpa ujazito.

“Baraza limeafiki kufukuzwa kazi Muuguzi huyo baada ya kujiridhisha kuwa alikiuka maadili ya utumishi wa umma na hata baada ya kusomewa hukumu hakukata rufaa kama sheria inavyoeleza, hivyo tumemfukuza kazi rasmi,” amesema.

Aidha, Mstahiki Meya ameongeza kuwa mtumishi mwingine, Rehema Mussa (Muuguzi katika Zahanati hiyo) amesamehewa na kurejeshwa kazini na atakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha miezi 6 baada ya kupatikana na hatia ya kutofika kazini kwa siku 37.

Amefafanua kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada ya mtumishi huyo kukiri kosa na kuandika barua ya kuomba msamaha huku akibainisha matatizo mbalimbali ya kifamilia ikiwemo ugonjwa yaliyopelekea kutokuwepo kazini kwa muda huo.

Akiongea kwa masikitiko, diwani wa kata ya Ifucha, Rose Kilimb, amesema kuwa mtumishi wa umma yeyote anapaswa kuwa kioo cha uadilifu katika jamii na sio kujihusisha na vitendo visivyofaa ikiwemo ubakaji.

Naye Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo, Christina Bunini, amewataka watumishi wote wa umma katika halmashauri hiyo kuzingatia maadili ya kazi zao na kufuata kanuni na taratibu katika kutekeleza majukumu ili kutoingia matatizoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles