23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mtumishi TRA, polisi wanaodaiwa kuomba rushwa kwa mfanyabiashara kizimbani

NA KULWA MZEE

-DAR ES SALAAM

MFANYAKAZI mmoja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na askari polisi wawili, wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kushawishi kupewa rushwa ya Sh milioni mbili na mfanyabiashara Ramadhani Tunzwe.

Washtakiwa hao ni askari H 4086 PC Simon Sungu, H 4810 PC Ramadhan Uwezi wa Kituo cha Polisi Osterbay na Charity Ngalawa ambaye ni mfanyakazi wa TRA.

Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Sophia Gula, aliwasomea washtakiwa shtaka linalowakabili mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Alidai washtakiwa wanashtakiwa kwa kushawishi rushwa, ambapo wanadaiwa Oktoba 29, 2016 maeneo ya Kimara Mwisho, wakiwa wafanyakazi wa TRA na polisi, walidai rushwa ya Sh milioni mbili kutoka kwa Tunzwe.

Washtakiwa wanadaiwa walidai rushwa hiyo kama kishawishi cha kuruhusu mzigo wake ambao unadaiwa ulikadiriwa kodi ndogo jambo ambalo lilikuwa chini ya wakubwa wao.

Washtakiwa walikana kutenda makosa hayo, na Jamhuri walidai upelelezi haujakamilika na hapakuwa na pingamizi kwa washtakiwa kupata dhamana.

Mahakama ilikubali kuwapa dhamana kwa masharti ya kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni tano. Washtakiwa walitimiza masharti ya dhamana, wako nje.

Juni 7, Rais Dk. John Magufuli alitoa maagizo kwa washtakiwa kuchukuliwa hatua baada ya kuibuka hoja Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kusema maofisa wa TRA waliomba rushwa kwa Tunzwe mwaka 2016 na alipokataa walishikilia mizigo yake kwa miaka mitatu hadi Aprili, mwaka huu alipoingilia kati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles