22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mtuhumiwa wa mauaji ya askari atiwa mbaroni

IGP Mangu
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Mangu

NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR

MAKACHERO wa Jeshi la Polisi Zanzibar wamefanikiwa kumtia mbaroni mmoja wa watuhumiwa wa mauaji ya askari polisi mmoja na askari mgambo katika Kituo cha Polisi cha Kimanzichana, Mkuranga mkoani Pwani.

Ofisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Inspekta Mohamed Mhina, amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Hamis Othman Mzee (44), maarufu kwa jina la Hamisi Mabunduki, mkazi wa Zanzibar pamoja na Dar es Salaam.

Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, ACP Juma Yusuf Msige, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kijiji cha Matale, Wilaya ya Chakechake akiwa mafichoni.

Kamanda Msige alisema taarifa za kiintelijensia zinaonesha kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni hatari, amekuwa akikabiliwa na kesi lukuki za matukio ya ujambazi wa kutumia silaha na alitoka rumande Mei 28 mwaka huu na tangu wakati huo mtuhumiwa huyo na genge lake amekuwa akiendeleza matukio ya kiuhalifu, yakiwemo uporaji na mauaji katika mikoa mbalimbali.

Kamanda Msige alisema Polisi wanaendelea na upelelezi ikiwa ni pamoja na kupata taarifa muhimu za watuhumiwa wengine wanaojificha ili watiwe mbaroni kukabiliana na mkono wa dola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles