24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Mtuhumiwa sugu wa mauaji mbaroni

NA ALLAN VICENT -Tabora

MTUHUMIWA sugu wa mauaji na uvunjaji nyumba aliyekuwa akisakwa kwa muda mrefu na Jeshi la Polisi mkoani Tabora, amekamatwa kutokana na msako mkali uliofanywa maeneo mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa kutokana na ushirikiano mzuri wa wananchi kwa jeshi hilo.

Alimtaja mtuhumiwa kuwa ni Juma Nassibu, maarufu ‘Juma Macho’ na kwamba anaendelea kuhojiwa.

Kamanda Mwakalukwa alisema msako unaendelea kwa weledi mkubwa maeneo yote ya mkoa  hadi hapo wenzake watakapokamatwa au kujisalimisha wenyewe.

Alisema katika msako huo, pia walifanikiwa kumkamata kinara wa wizi wa pikipiki mwenye mtandao mpana mikoa ya Tabora, Mwanza, Shinyanga na Mara.

Kamanda Mwakalukwa alisema baada ya mahojiano na polisi, mtuhumiwa alikiri kuhusika na mtandao huo wa wizi wa bodaboda na kubainisha  tayari ameiba zaidi ya nane katika mikoa hiyo.

Baada ya kukamatwa, alikutwa na vitu mbalimbali ikiwemo pikipiki tatu zenye namba za usajili T 615 AVE aina ya SanLG, MC 977 AAB na T 791 ATN, huku pikipiki yenye nambari MC 274 ikiwa inabadilishwa injini yake.

Alitaja vitu vingine ni radio sabwoofer moja, TV tatu flat screen, deki moja, baiskeli mbili na magodoro mawili.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles