24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 29, 2023

Contact us: [email protected]

Mtoto waRuge atoa mazito

Na EVANS MAGEGE – Dar es Salaam

MTOTO  mkubwa wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group (CMG), marehemu Rugemalira Mutahaba maarufu Ruge, Mwachi Ruge, amemwombea msamaha baba yake kwa watu ambao aliwakosea kipindi cha uhai wake.

Mwachi alitumia fursa hiyo jana wakati akisoma wasifu wa marehemu baba yake katika shughuli ya kumuaga iliyofanyika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.

Akisoma wasifu huo taratibu huku machozi yakimtoka, Mwachi alisema baba yake alikuwa mshindani halisi na anatambua kwa biashara yoyote kibinadamu kwa namna moja au nyingine huwa kunatokea kukwazana.

Kauli hiyo ilionekana kuwasababishia zaidi uchungu baadhi ya watu ambao baadhi walishindwa kujizuia na kuangua kilio.

Mwachi alikwenda mbali zaidi akisema kwa niaba ya familia yao anawasamehe wale wote ambao walimkosea Ruge.

Alisema nia ya familia yao ni kwenda mbele kwa pamoja, kupendana na kuheshimiana.

“Familia imeishakubali kwamba Ruge hakuwa …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,259FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles